Kwa hili wabunge wa Dar hamuwezi kujiepusha kuwa MUWANAFIKI!!

Mringo

JF-Expert Member
Jun 23, 2010
320
100
Juzi Mh.Magufuli alipopandisha nauli ya kivuko muling'aka na kuweka tofauti za kichama pembeni huku mukidiriki kumtaka aombe radhi..Tena hii ni ishu ambayo htuwezi kusema ina hatarisha maisha ya mtu...Ahsante sana Magufuli kwa kuonyesha kuwa wewe ni mtu makini na sio bendera-fuata upepo...
Hivi karibuni madkari muhimbili wakagoma wakidai haki yao ya msingi ambayo hata kama ingekua ni wazizi aliyenyimwa haki ile basi angediriki kutundika daluga...cha ajabu wakalipwa haki yao na kisha kufukuzwa....nakuacha maisha wananchi yakiteketea mmoja mmoja..
Cha ajabu sasa hawa wanaojiita wabunge tetea wananchi hakuna aliyejitokea na kuitaka wizara iache kuwaghilibu watanzania wamkaa kimya tu hata hawaoni....Nilitarajia kwa walivyomjia juu magufuli basi wangeshaendesha mgomo wakushinikiza serikali iwarudishe mara moja madaktari..
Hivi ninyi wabunge tuwaaminije kuwa hamkua na ajenda ya siri ya kumdhalilisha magufuli ni vile tu mukakuta naye ni kisiki cha mpingo kisichosikia makali ya panga.....
Badilikeni munatutia hasira
 
Magufuli ni mtu mmoja tangible, wakati serikali iliyowafukuza madaktari kupitia Wizara iko intangible and vast!
 
Back
Top Bottom