Kwa hili Viongozi wa Dini tuungeni mkono.

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Habari wanajamvi.

Naomba nianze kwa kukumbusha jambo la msingi ambalo sote tunapaswa kujua nalo ni,

"Kuwa karibu na Mwenzi wako ni haki ya Kimsingi kabisa kwa Binadamu yeyote (Conjugal right)"

Ila ninajiuliza kwa nini Serikali haitaki kuruhusu UHAMISHO ili jambo hili la msingi liwe katika msingi wake?.

Kuna watu wanataka kuhama ili kuwafuata wenzi wao kule walipo kusudio lao ni kupata conjugal right lakini Serikali hailioni hili.

Watu wengi wamesema juu ya hili lakini Serikali imeweka pamba masikioni.

Binafsi niwaombe Viongozi wa Dini wakamee jambo hili la Serikali kuwanyima watu conjugal rights.

Viongozi wa Dini mkemee hili ili Serikali iruhusu UHAMISHO kwa ajili ya kuwafanya Waumini walio kula kiapo cha kuwa pamoja kama MUME na MKE wapate kufurahia maisha yao ya Ndoa.

Msikubali hali hii iendelee ili Mapenzi ya MUNGU yatimizwe.
 
Back
Top Bottom