Kwa hili polisi Arusha mnatutia mashaka

Kwa hili polisi Arusha mnatutia mashaka

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,210
Reaction score
4,178
Ndugu wana JF,

Wenzangu na wanachama wa CHADEMA wapenzi na washabiki nawapa pole kwa tukio na msiba wa wenzetu walio poteza maisha yao,jana Soweto Kaloleni, nilishngazwa na jeshi la polisi kwa kitendo chao cha kuwapiga watu mabomu na risasi za moto, nilijiuliza maswali haya; [1]kulikua na ulazima gani jeshi la polisi kupiga mabomu watu na risasi za moto kutumika
[2]nimepata mashaka labda jeshi la polisi lilitaka kufanikisha mtuhumiwa atoroke bila kukamatwa
[3]ilitakiwa jeshi la polisi lishirikiane na wananchi kufanikisha kumkamata mtuhumiwa kama walivyo fanya kule Olasite, sasa tunapata mashaka kwamba jambo hili lilipangwa, naomba tutafakari pamoja wana JF wenzangu juhu ya jambo hili la jana naomba michango yenu,
 
Hiyo ni kweli ILA nawashangaa POLISI kwenda kinyume na dhana ya POLISI JAMII kwa kumtorosha mtuhumiwa na kuwageuzia kibao raia wema!
Hii kazi mie hata wana-ukoo wetu tutapanga kuisusia...SI KAZI YA HESHIMA!
 
Bomu linalipuka watu wanataharuki wanakimbia kuokoa maisha yao.......askari wanapga mabomu ya machozi na risasi hewani..........kumtawanya nani? kumdhibiti nani? Kumlinda nani?

Kijana aliye rusha bomu alionekana...........lakini mabomu ya machozi, risasi hewani, nani angemfuatilia kumkamata?.........was it a tactic.....kwamba we lipua then sisi puuuuuuuuuu..........paaaaaaaa aaaaaaaa...........kabouuuuuuu uuuuuuuuuum? Hapa chenga tu kwakweli, cjui hao askari walipotoka maofsini kwao kuja kulinda amani walipata muda wa kujadili na kupeana mawazo juu ya aina za matukio yanayoweza kutokea na namna ya kuyakabili? hii inatisha sana........
 
Ndugu wana JF,

Wenzangu na wanachama wa CHADEMA wapenzi na washabiki nawapa pole kwa tukio na msiba wa wenzetu walio poteza maisha yao,jana Soweto Kaloleni, nilishngazwa na jeshi la polisi kwa kitendo chao cha kuwapiga watu mabomu na risasi za moto, nilijiuliza maswali haya; [1]kulikua na ulazima gani jeshi la polisi kupiga mabomu watu na risasi za moto kutumika
[2]nimepata mashaka labda jeshi la polisi lilitaka kufanikisha mtuhumiwa atoroke bila kukamatwa
[3]ilitakiwa jeshi la polisi lishirikiane na wananchi kufanikisha kumkamata mtuhumiwa kama walivyo fanya kule Olasite, sasa tunapata mashaka kwamba jambo hili lilipangwa, naomba tutafakari pamoja wana JF wenzangu juhu ya jambo hili la jana naomba michango yenu,

Ni vizuri tukajiuliza ushindi wa kishindo uliongelewa katika uzi huu ni upi? (https://www.jamiiforums.com/chaguzi-ndogo/469001-ccm-kushinda-kwa-kishindo-kata-zote-nne-arusha.html )
[h=2]na ile ya kazi ya Mungu tuu, ndio kazi iliokamilika (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/466791-kazi-ya-mungu-tuu-ndio-kazi-iliokamilika.html)[/h]
 
Niliandika Thread kama hii lakini imegoma kuonekana, sijui tatizo nini. Polisi wetu tuna maswali mengi juu ya kilichotokea jana na yanayoendelea kutokea katika chaguzi hizi za madiwani. Hakukuwa na ulinzi katika mkutano wa Chadema? Kama ulikuwepo inakuwaje aliyerusha bomu asikamatwe? Bomu limerushwa watu wamejeruhiwa na wengine wamekufa kwanini polisi wapige mabomu ya machozi na risasi za moto? Polisi walilenga kumwokoa mtu aliyerusha bomu asikamatwe? Au kuwadhuru viongozi wa Chadema hasa Mh. Mbowe na Lema? Tunahitaji majibu ya maswali haya, vinginevyo Watanzania tunaamini polisi mmeshirikiana na ccm kupanga haya matukio. Na ndiyo maana polisi ni wazito kuchukua hatua.
 
"Our homeland security is poor if not weak, and if this is a case....."
Je, tunahitaji kuendelea kuwa na jeshi hili la polisi?
Je, kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na waziri wa mambo ya ndani?
Je, kifanyike nini sasa ili kunusuru maelfu kama siyo mamia ya watanzania wanaoendelea kuuwawa siku?
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kusoma baadhi ya post kuhusu tukio la bomu la soweto na yaliotokea baada ya hapo nimebaki na maswali juu ya ufanisi na nia halisi ya jeshi la polisi, hasa baada ya kuelezwa kuwa askari walilipua mabomu ya machozi, na kupiga risasi hewani mara baada ya bomu hilo kulipuka.

1. Baada ya bomu kulipuka wananchi walikuwa wakikimbia huko na huko kwa mshtuko mkubwa na kuhofia maisha yao.
Ilihitajika kweli kulipua mabomu na kupiga risasi hewani kama njia ya kuwatawanya wananchi hao waliokwisha tawanyika kwa mshtuko huo?

2.aliyerusha bomu yasemekana alionekana na walimwelezea kwa mavazi yake na mahali aliposimama kabla ya tukio. Naamini wapo wananchi ambao wangemkimbiza kwania ya kumkamata kama ilivyotokea ktk mlupuko wa kanisa....je polisi hawaoni wana lakujibu ktk kumpatia mwanya mtuhumiwa atoroke?

3. Hivi hata baada ya matukio meeeeengi tuu ya uvunjifu wa amani ktk mikutano ya cdm..polisi wanao kwenda kusimamia hali ya usalama ktk mikutano huwa wanapata muda wa kujadili ni aina gani ya matukio ya nayoweza kutokea na namna tofauti ya kuyakabili kila moja?

Naleta hayo tujadili kwania kuu ya kulishauri jeshi letu la polisi
 
Ndugu wana JF,

Wenzangu na wanachama wa CHADEMA wapenzi na washabiki nawapa pole kwa tukio na msiba wa wenzetu walio poteza maisha yao,jana Soweto Kaloleni, nilishngazwa na jeshi la polisi kwa kitendo chao cha kuwapiga watu mabomu na risasi za moto, nilijiuliza maswali haya; [1]kulikua na ulazima gani jeshi la polisi kupiga mabomu watu na risasi za moto kutumika
[2]nimepata mashaka labda jeshi la polisi lilitaka kufanikisha mtuhumiwa atoroke bila kukamatwa
[3]ilitakiwa jeshi la polisi lishirikiane na wananchi kufanikisha kumkamata mtuhumiwa kama walivyo fanya kule Olasite, sasa tunapata mashaka kwamba jambo hili lilipangwa, naomba tutafakari pamoja wana JF wenzangu juhu ya jambo hili la jana naomba michango yenu,

Polisi ndio waliozuia mtuhumiwa asiikamatwe. Gazeti la mwananchi linaripoti katika habari yenye kichwa,
[h=1]Ugaidi tena Arusha, bomu lajeruhi na kuua kuwa, "Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki."[/h]Dalili za serikali ya CCM kutaka kuzuia uchaguzi wa Arusha zilianza kuonekana toka Tume ya uchaguzi ilipotangaza uchaguzi huo. Mkuu wa mkoa wa Arusha alianza vituko kwa kuhusisha mbunge wa Arusha na mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha uhasibu na baadaye kumkamata mbunge huyo kwa kisingizio kuwa alichochea vurugu. Mbunge huyo alikamatwa usiku kwa askiari wa polisi kuruka ukuta wa nyumba yake.

Haya yote yalikuwa ni ili wananchi wa Arusha wafanye vurugu ili ionekane kuwa Arusha haina Amani hivyo waishauri tume izuie uchaguzi.

Kutaka wananchi wafanye fujo pia inaonekana pale tume ya uchaguzi ilipokataa kutangaza uchaguzi kwenye kata ile iliyokuwa wazi baada ya Mawazo kuhamia CHADEMA. Hii nayo iliachwa maksudi ili wananchi wa Arusha waandamane na polisi wawafanyie vurugu ionekane kuwa Arusha hakuna amani. Hata hivyo CHADEMA walikuwa na busara hivyo hawakufanya lolote lenye kuruhusu kufanyiwa fujo.

Kitendo cha jana baada ya mlipuko badala ya polisi kufanya kazi ya uokozi na kuwaelekeza watu wao wakaanza kulipua mabomu kinaashiria ni kwa jinsi gani CCM na serikali ya mkoa hawako tayari uchaguzi huu urudiwe.

Kama CCM hawahusiki na tukio la jana, utaona mtuhumiwa atakamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani na kesi kuanza mara moja. Kama CCM inahusika, watakamatwa vijana wataonyeshwa kwenye vyombo vya habari ila hutasikia kesi inasikilizwa.
 
Polisi wanaelewa kila kitu,baada ya bomu kulipuka polisi walikuwa wanarusha mabomu kila kona hata mtu aliyerusha alishashikwa akatoroka.
 
Lengo ni moja tu ccm ipumzike haikubaliwi tena inalazimisha kupendwa?
 
Pole kwa wale wote walioathirika kwa namna moja ama nyingine maana hayo sio mambo ya kumwombea Mtanzania mwenzako.

Na pili pongezi kwa waheshimiwa Mbowe, Lema na viongozi wengine wa CDM waliokuweko katika tukio. Maana safari hii hawajaja na kauli za haraka za shutuma dhidi ya CCM kama tamko la chama na wao wakiwa kama watu waliokuwepo kwenye mkutano huo ndio ukakamavu wenyewe huo maana si muda muafaka wa kuanza kutoa isia halafu mahala ambapo CDM ina support kubwa inavyooneka the situation could have spiraled out of control or worsen.

Lakini kwakweli ni mambo ya kushangaza sana it doesn't make sense kwa serikali kwenda kupiga bomu mkutano ulikokwisha kwa nia ya kuwatishia wananchi kwenye chaguzi it just doesn't add up on the effect of the election outcome. Unless nia na madhumuni ni kuwaondoa viongozi wa CDM that is the only motive ambayo inaweza tupa sie vilaza wanje za siasa za Tanzania any sense. Lakini for fear tactics it just doesn't add up.

Na kama wengine wanavyotushauri si sawa kuanza kunyoosheana vidole wakati hata uchunguzi bado na wala testimony za watu waliokuwa kwenye mkutano bado, maana hapa kama kuna mkono wa nje kitakacho fuata nadhani ni kumwondoa kiongozi mmoja wa juu wa CDM kama sio sasa chaguzi kuu huko mbele hili kufanikisha malengo yao ya nchi kuwa na matatizo.

Ni busara sana hizi siasa za uchochezi na kutumia hisia za watu vyama vikuu vya siasa vingeziacha maana vinawapa mwanya watu wa kuwagombanisha na bora sasa watu warudi kwenye sera na kutafuta kura kupitia matatizo ya wananchi kuliko kukuza chuki, hizi habari za udini, kutembeza watu waliomwagiwa tindikali kuitana magaidi zitatupeleka pabaya na ziwe marufuku especially kauli kama za tulianza na mungu tutamaliza na mungu where on politics does god fit.
 
Pale kanisani hawakutumia mabomu wala risasi. Je baada ya tukio la kanisani wamejifunza kuwa kunapokuwa na tukio kama hilo watumie mabomu ya machozi? Inashangaza, inahuzunisha, inatia wasiwasi.
 
Pole kwa wale wote walioathirika kwa namna moja ama nyingine maana hayo sio mambo ya kumwombea Mtanzania mwenzako.

Na pili pongezi kwa waheshimiwa Mbowe, Lema na viongozi wengine wa CDM waliokuweko katika tukio. Maana safari hii hawajaja na kauli za haraka za shutuma dhidi ya CCM kama tamko la chama na wao wakiwa kama watu waliokuwepo kwenye mkutano huo ndio ukakamavu wenyewe huo maana si muda muafaka wa kuanza kutoa isia halafu mahala ambapo CDM ina support kubwa inavyooneka the situation could have spiraled out of control or worsen.

Kwa hiyo BOMU limelipuliwa na nani kama siyo sisiemu?! .... Kwa nini mkutano wa CCM haukushambuliwa?
 
Naamini Polisi wanujua ukweli utasikia rpc kapandishwa cheo si kama iringa hakuna jipya
 
Kwa hiyo BOMU limelipuliwa na nani kama siyo sisiemu?! .... Kwa nini mkutano wa CCM haukushambuliwa?
Kuna sababu gani ya kupiga bomu mkutano wa chama tawala hiwapo nia na madhumuni ni kuleta mfarakano, kwenye mkusanyiko wa CCM kama itatokea hali mbaya na kukawa na matatizo mwishowe polisi wakatumia excessive force, sanasana wananchi watasema ukiona hivyo ilibidi polisi kufanya hivyo (na CCM hawato toa shutuma dhidi ya chama kingine bila ya ushahidi) kwa hivyo kama mtu alikuwa na nia mbaya mpango wake mzima utaanza kuaribika mapema CCM aitoruhusu wanachama wake wafanye fujo za aina yeyote (be it kwa uwaziwazi).

Lakini kupiga bomu mkusanyiko wowote ambao auna direct links/ties na CCM according to opposition past accusations, will sure cause the government being tied of foul play hata ambapo clearly there is no evedince to suggest so nor the motive to act so like in this instance.

CCM inauwezo wa kuiba kura, inauwezo wa kufanya upigaji kura ukawa wa tabu sana kwa wapigaji kura;maana sidhani kama kura za udiwani zina international observers na ina uwezo wa kuzuia mkutano wenyewe eti ichague kupiga bomu mkutano ulioisha kwa nia gani especially ukizingatia ni juzi serikali imetoa tamko utalii umeleta over a million watalii therefore even economically aina sababu ya kutaka arusha isitwalike? Kitendo cha kufanya yaliyotokea jana sanasana itakuwa imeamua kujinyima kura tu zaidi. Therefore if the issue was about electoral outcome, CDM in bombing their gathering has more to gain than CCM that is just commonsense.

Lakini we cant assume people will resort to such devilish acts for the sake of controlling Arusha (who knows may be they can, maana baada ya tukio tu watu wengine wameshaanza kuilaumu serikali wakati hawapo hata nchini), sasa hizo facts wamezitoa wapi.

Hila sisi wengine tunaona hili swala ni gumu sana na linaweza kuwa na huge implications huko mbele hivyo ni bora uchunguzi ufanyike independently ikiwezekana hili kukata mzuzu wa fitina walianza na kanisa na waumini wasio na hatia, sasa wanaanza kuichokoza demokrasia yetu na kuwaua wasio na hatia i dont think we can afford to accept unsubstantiated allegations zisizo na kichwa wala miguu considering the long term stability of our nation is at stake.
 
Ndugu wana JF,

Wenzangu na wanachama wa CHADEMA wapenzi na washabiki nawapa pole kwa tukio na msiba wa wenzetu walio poteza maisha yao,jana Soweto Kaloleni, nilishngazwa na jeshi la polisi kwa kitendo chao cha kuwapiga watu mabomu na risasi za moto, nilijiuliza maswali haya; [1]kulikua na ulazima gani jeshi la polisi kupiga mabomu watu na risasi za moto kutumika
[2]nimepata mashaka labda jeshi la polisi lilitaka kufanikisha mtuhumiwa atoroke bila kukamatwa
[3]ilitakiwa jeshi la polisi lishirikiane na wananchi kufanikisha kumkamata mtuhumiwa kama walivyo fanya kule Olasite, sasa tunapata mashaka kwamba jambo hili lilipangwa, naomba tutafakari pamoja wana JF wenzangu juhu ya jambo hili la jana naomba michango yenu,

Ungekumbuka yule mtuhumiwa aliyemchinja marehemu Mbwambo kule USA River kwa ushaidi uliojitosheleza na kuonyesha vidhibiti vyote mtuhumiwa mwenyewe wala usingesumbuka kujiuliza haya. Kwani si aliondokea mikononi mwa polisi hawahawa?
 
Lakini we cant assume people will resort to such devilish acts for the sake of controlling Arusha (who knows may be they can, maana baada ya tukio tu watu wengine wameshaanza kuilaumu serikali wakati hawapo hata nchini), sasa hizo facts wamezitoa wapi.

Hila sisi wengine tunaona hili swala ni gumu sana na linaweza kuwa na huge implications huko mbele hivyo ni bora uchunguzi ufanyike independently ikiwezekana hili kukata mzuzu wa fitina walianza na kanisa na waumini wasio na hatia, sasa wanaanza kuichokoza demokrasia yetu na kuwaua wasio na hatia i dont think we can afford to accept unsubstantiated allegations zisizo na kichwa wala miguu considering the long term stability of our nation is at stake.

Sasa wewe ndugu yangu unataka nani alaumiwe?!!... Kwani nini CCM na serikali yake isilaumiwe?!!!... Uchunguzi na ripoti ya waliorusha bomu kanisani upo wapi?... Kama hisia ni kwa Al shababu,... Ni nini hasa kiwasukume kufanya hujuma hii?!!!... kwa CCM iko wazi wanasaka ushindi hata kwa njia haramu!.. Na hili wamekiri kupitia shonza, mtela na mwigulu!!!!!!!!!.
 
Back
Top Bottom