Kwa hili nililosikia simuungi mkono

madala mujipa

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
1,417
861
Salaam kwenu
Hapa ninapopita kwa muda huu ni uchochoroni mwa nyumba nasikia sauti ya mwanamke akigomba kwa sauti ya juu,nimevutika na anachosema wewe baba iddi umezoea ukiona ndugu yangu amekuja tu unaanza visa unataka kuhesabu vipande vya nyama ili uanze ugomvi unipige kwanini hukuingia jikoni ukapika

Nikaamua kutoa sigara nivute kuzuga mara baada ya kimya kingi nasikia sauti ya kiume ikijibu si pesa nimetafuta mwenyewe na nyama nimenunua lazima tule kwa bajeti na sitaki tabia ya kunichonganisha na ndugu za kama vipi uwanja wote nitaupanda mbigili na wasikanyage tena

Nikaamua kuondoka kuwaacha wakiendelea na malumbano yao

Lakini kwa hili nililosikia baba iddi sipo pamoja nae

Sijui wadau mnaichukuliaje hii
 
Najaribu kuioanisha na 'gongo' naona kama kuna......
 
Mambo ya watu ww yanakuhusu nini mkuu?

Acha apande mbigiri km anadhani akifa atajizika

Mkuu;
Kifo cha baba Iddi na ujio wa mashemeji wake vina uhusiano gani?? Kwani hao mashemeji ndio wachimba kaburi tu walioko??
Sikilizeni, nyiye ambao hamjawahi kuzongwa na mashemeji hamjui mapito anayo pitia baba Iddi. Kwani alioa mji wote au alimuoa Mwajuma?? Pongezi baba Iddi, panda mbigili na huyo mkeo akileta ngebe mfungie hao ndg zake arudi nao kwao. Tuone watakula nini huko. Kazi hawafanyi, wanachojua ni kula minyama tena wanataka wale finyango sawa na aliyeleta. Pambafuuu
 
Mkuu angalia usije tobolewa sikio shauri ya kusikiliza ya majumbani mwa watu..!! Ohoo shauri yako..!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom