gilmanywele
Member
- Aug 17, 2015
- 53
- 15
Moja ya mambo ambayo naona maamuzi yake hayakuridhisha ni suala la hawa wadogo zetu wa UDOM. Hivi ilishindikana nini kuruhusu hao wanafunzi kumaliza masomo yao ila wakazuia usajili mpya wa wanafunzi hao kuanzia mwaka huu..!?
Sidhani kama mwanafunzi aliyepata division one-three O'level ambako alikuwa na masomo mengi zaidi, kwamba akifundishwa masomo mawili au matatu kwa miaka mitatu ya Diploma atashindwa kufundisha wadogo zake wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Maana hata walioenda A'level kwa miaka miwili bado wamekuwa wakisaidia ufundishaji japo baadhi hupungukiwa kiasi skills za ufundishaji tofauti na hawa wa diploma.
Au serikali inakwepa "mzigo" kuambiwa baadaye kuwaajiri na ilhali bado kuna walimu wengine hawajaajiriwa?
Ambao walikuwa na division four inakisiwa idadi yao kuwa 88. Sasa hawa ni wachache mno kati ya wanafunzi wote. Sidhani kwamba wengi wa wanafunzi waliopata division one na two walienda kwenye diploma hii. Inammanisha division three ndio wengi. Sasa, wangeamua kuendelea na masomo ya A'level, shule zetu zilikuwa na uwezo wa kuwamudu kwa idadi yao!?
Mara fedha ndo tatizo. Ndio nini sasa hiyo?. Pamoja na juhudi kubwa za kuzuia matumizi yasiyo ya lazima, ni dhahiri serikali ina fedha za kumudu malipo hayo. Fedha kisiwe kigezo cha kutowalipa walimu ikizingatiwa fedha hizo zilikuwepo katika bajeti ya serikali kwa mwaka uliopita. La kujiuliza ni hili; hizo fedha zilienda wapi hadi walimu wa hao wadogo zetu wakaingia katika migogoro?
Sikuielewa serikali hii kwa kweli.