Kwa hili la panga pangua viongozi Rais Samia atapoteza mvuto kwa Chama na kwa Wananchi

Msifikiri makonda aliposema viongozi wengi ni wanafiki aliropoka tu alimaanisha sana
Mimi niwambia 2025 ccm itakuwana mgombea mwigine kabisa mpaka sasa washauri wanampoteza kisomi wengi watz imani imepungua kwa 95%
Ngoja twaweza waingie kazini mwone
 
Inaonekana nyumbani kwako unawalaumu watoto kwa maamuzi yako mabovu.
 
Nakubaliana na wewe P lkn kuna tatizo mahala. Haiwezekani kufanya teuzi kwa majaribio(sumu haionjwi).

kuna kundi fulani linalompotosha kwa manufaa yao.
Lipo ni kundi la wahafidhina wanamuingiza maza chaka, Maza akiisha jaa kwenye 18 yao, 2025 watamtosa!.
P
 
Idd Amini alipokuwa anapanda ndege kukimbilia Libya,

Alitoa vitisho ambavyo wanajeshi wetu wangesikia wote wangekimbiana.

Nakuelewa unachokimaanisha, unaamua kufa na tai shingoni.
 
Nimuda wake na Katiba inamruhusu kufanya hivyo, na washauri wake wamekubaliana, anaona inamsaidia kwenye uongozi wake, mwacheni apambanie muda wake kuongoza nchi si jambo dogo. Si dhani kama ni dhamira yake kufanya mabadiliko kila mara, changamoto inayoonekana hapa ni aina ya watu wanaomzunguka ni tofauti na matarajio yake.
 

Sasa kaka, kweli unaona chini ya Uongozi wake kuna anae ogopa!? Huoni wanaotoswa baada ya miezi wana rudi tena, mbaya wanaotoswa ni kwa kashfa lakini wanarudi tena mfano Chongola.

Sidhani kama Mobutu ni mfano mzuri wa mfumo huu, hili linalofanyika liko mbali kabisa na unayo sema.. sioni vikifanana.. maana hao wanaobadilishwa badilishwa hamna kitu wanafanya wanapo toka.. Mfano Mhede au huyo Kindambwa, wamesha kaa nafasi ngapi!?
 

Ina maana tutawalaumu walio mzunguka, yeye hana fikra zake?! Hana utashi na fikra zake za kuona kipi ni kibaya kipi ni kizuri! Akiwa kama Rais hana nafasi ya kukataa lililo baya!?
 
Idd Amini alipokuwa anapanda ndege kukimbilia Libya,

Alitoa vitisho ambavyo wanajeshi wetu wangesikia wote wangekimbiana.

Nakuelewa unachokimaanisha, unaamua kufa na tai shingoni.
Hakuna, cha sijui nani alifanya nini, wap na tai...
Kazi lazima ifanyike...🐒

ukweli usemwe bila mbambamba, Comrade Dr SSH ni mahiri na ni madhubut mno katika uongozi wa nchi. hayupo na hakuna wa kumtisha wala kumuyumbisha kwa namna yoyote ile.

waTanzania kwa umoja na kwa maelfu na mamilioni yao, wanamuunga mkono, wanampenda, wanamfurahia nae bila hiana anawapa tabasamu na anawafurahisha kwenye maji,elimu,afya, kilimo, biashara n.k🐒

na uteuzi huu unalenga kuwafurahisha wanainchi zaidi 🐒
 
Lipo ni kundi la wahafidhina wanamuingiza maza chaka, Maza akiisha jaa kwenye 18 yao, 2025 watamtosa!.
P
Sasa kwanini asitafute historia ya hao Wahafidhina kabla ya kufanya teuzi??? Mimi ningemshauri aachane na Uchawa kwani ndiyo unaochangia haya yote.

Hebu fikiria alipomteua Makonda kuwa Mwenezi wa CCM Chawa walimpongeza na kumsifia. Amemtoza kwenye Uenezi Chawa wale wale wamerudi tena kumsifia kwa kumtoza.
 
Umempaka mafuta mazuri kwa mgongo wa chupa!
 

Daah
wewe jamaa uko vizuri sana.
 
Umempaka mafuta mazuri kwa mgongo wa chupa!
hakuna chupa yoyote hapa wala mgongo wake 🐒

na huu ni mwanzo na haya anayofanya hivi sasa ni kwa uchache tu, japo mengi ni bayana na yanaonekana mchana kweupe 🐒

bila kumuonea mtu haya wala aibu, tutawaeleza waTanzania kinagaubaga mambo muhimu ambayo CCM chini ya Dr.SSH wanafanya kwa maslahi mapana ya waTanzania 🐒

ili hatimae wale wa porojo na stori za sijui nini, nao wakataliwe hadharini kwenye sanduku la kura, Lakini kidemokrasia 🐒
 

Unavyo ongea ni unanikumbusha kitabu kimoja cha Lelo Mmasi.. cha Mimi na Rais namna wapambe walivyokua wanamsifia Rais Costa wa Stanza… unajua kusifia ila unasifia kwenye hamna… unasema ukweli wa uongo.
 
Kama jpm mliimwita mshamba huyu tumwiteje sasa maan serikali tu ameshindwa kuunda kwa miaka 3 kipi anakiweza kwa sasa
 
Unavyo ongea ni unanikumbusha kitabu kimoja cha Lelo Mmasi.. cha Mimi na Rais namna wapambe walivyokua wanamsifia Rais Costa wa Stanza… unajua kusifia ila unasifia kwenye hamna… unasema ukweli wa uongo.
kama ambavyo Rais asivyobabaika na wakisoaji wake na wale wanamuhujumu kwa makundi...

mimi pia sina mbambamba yeyote na mwenye maoni au mtazamo tofauti na ukweli huu bayana sana, kuhusu jitihada za Rais, comrade SSH katika kuchochea maendeleo kwa kufanya mabadiliko ya uongozi maeneo na sekta mbalimbali humu nchini...

Riwaya, hadidhi na simulizi zibaki tu kama kitu cha kuliwaza au kukupa matumaini au burudani kwako na kwa wengine waonao zipenda,
Acha wengine tusonge kwa style hii 🐒
 
Ccm ilipoteza mvuto toka uchaguzi wa 2010, nguvu ya Dola ndio imebaki mbeleko pekee ya wao kutangazwa washindi kwa shuruti. Kwahiyo si kweli kuwa ccm ipoteza mvuto kutokana na hizi teuzi za rais, Bali ilishapoteza mvuto muda mrefu.
Nakubaliana na wewe sanaa kwenye hili...hawa inabidi watolewe kwa mtu.....
 
Katika mchezo huu wanaotoswa kabisa wapo lakini wachache sana. Lengo kuu la teua, tengua, hamisha ni kuwaaminisha wananchi kuwa Rais anafanya kazi kudhibiti watendaji wake.

Wananchi huamini kuwa utendaji mbovu husababishwa na watendaji. Wrong. Hawa hawana uwezo wa kupitisha maamuzi makubwa - katika nchi hii.
 
Mimi nauliza wanapata saa ngapi muda wa kutumikia wizara zao au nafas zao leohuku kesho kule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…