jembepori
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 618
- 193
Ndugu watanzania, ni hatari sana kwa nchi kama yetu ya Tanzania kupitia tulichopitia kuhusu mauaji tena ya kuchinja watu zaidi ya wiki mbili mfululizo ikifungwa kazi na mauaji ya watu nane (8) waliochinjwa jijini Tanga kwenye eneo lile la mapango ya amboni.
Kilichosababisha niandike haya ni kuhusu haya mauaji kuwa yalitarajiwa lakini cha kushangaza viongozi wote wa mkoa walikuwa WAKIPUUZA TU!! Wananchi walianza kwa kulalamika kuwa kuna magaidi kwenye mapango yani mpaka watu wanaongea kwenye radio kuwa wanahofu na mambo yanayoendelea kwenye mapango lakini viongozi wa mkoa walikanusha na kusema hakuna gaidi wala jambo baya linaloendelea amboni.
Hali iliendelea hivyo leo tunaona na kusikia ndugu zetu wa Tanga wakilalamika kuwa hapa kuna ugaidi unaendelea, wakuu wa vyombo vya usalama na mkoa wanakuja na kusema ni majambazi tu yani hawachukulii jambo kiuzito unaopaswa kiasi kwamba ilikuwa inatupa shida hata sisi tulio huku mbali kwa kujiuliza maswali mengi.Hivi hawa viongozi ni mpaka watu wauawe ndiyo wachukue hatua?
Ikumbukwe kuwa mwaka jana kama siyo mwaka juzi kulikuwa na dalili za kuwepo kwa ugaidi kwenye hayo maeneo, kukutwa kwa bendera nyeusi zenye maandishi, kuuawa kwa baadhi ya polisi waliokuwa kwenye mapambano dhidi ya wahalifu hao na mpaka kulikuwa na clip inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kundi flani la kigaidi likimuonya Rais kuwa hawawaogopi hao polisi wake. Ingawa weeeengi walibeza na kujaribu kufunikafunika lakini zikianza kuonekana dalili kama zile kwanini hawa viongozi wetu na watu wa usalama wasishtuke mapema na kuchukulia kwa uzito mkubwa ili kuepusha madhara makubwa zaidi kwa wananchi?
Sasa majuzi wananchi wakawaona watoto wageni hivi, wakiwa wanatembea lakini hawayajui vizuri yale maeneo, wakaamua kwenda kutoa taarifa polisi na polisi wakaja wakawachukua watoto yaani kirahisi tu halafu wakakaa kimya na kuona kuwa ni sawa tu, huku wakijua kuwa kuna mtoto mmoja kawatoroka, kaenda wapi? wao hawajali na hawatuambii mpaka sasa hao watoto ni akina nani na wanataka nini hapo kwenye maeneo ya mapango.
Matokeo yake usiku wake wa kuamkia juzi wenye watoto wao wakaanza kuwatafuta watoto wao na walipowakosa wakaamua kuwachinja watu wote waliotoa taarifa za kukamatwa kwa watoto wakiwachukua mmoja mmoja kutoka kwenye familia zao tena mida ya usiku(shuhuda za familia zao)
Sasa baada ya watu kuchinjwa ndiyo unasikia Jeshi laingilia kati, kamati ya ulinzi yajifungia!! kamati gani hii? Hii kamati iliyoshindwa ku anticipate danger yani mpaka tukio linatokea tena mahala ambapo community cooperation ni kubwa kiasi kwamba taarifa wala hutafuti suala hili linaumiza sana. Tena linaumiza sana kwani kama wao wakishindwa kutulinda tutafanyaje? Tunawapeleka mafunzo ya gharama sana, tunawagharamia kila mwezi ila kufanyia kazi taarifa zetu kwa uzito ule tunaouona sisi hawawezi!!
Hii ni kashfa kubwa sana kwa kamati nzima ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Tanga.
Naandika kwa uchungu sana maana unaweza kunibeza ILA HUWEZI BEZA HOFU ILIYOJAA NDANI YA MIOYO YA WATU WANAOISHI MAENEO HAYO KWA SASA.
Ni rahisi sana kwa mtu mwenye ulinzi nyumbani kwake aliyepuuzia taarifa ambazo wao wangeziita za kiintelijensia toka kwa wananchi mpaka watu wanachinjwa leo kuwaambia watu msiwe na hofu akadhani hiyo hofu imekuja ghrafla, hapana hofu imetengenezwa na wao viongozi kwa kuruhusu haya kutokea na sidhani kama kuna mtu atakamatwa hapo kwenye huo msako wao wa mchana maana sidhani kama hao waharifu ni wajinga kiasi hicho.
Ni lazima mtu fulani awawajibike katika hili na mtu huyo anatakiwa awe ni kiongozi na wenyewe wanajifahamu, haiwezekekani watu kuchinjwa na siyo kwa bahati mbaya kwa maana dalili zilionyesha na bado zinaonyesha hatari iliyopo tanga hasa maeneo ya amboni halafu we kiongozi bado upo tu, unamuongoza nani?
Unajua nini jukumu la kiongozi la kwanza kwa watu wake? Hapa hata Rais hatakiwi kumuachisha mtu kazi ila Utashi tu unaonesha kuna mtu anatakiwa kuomba kustaafu kazi hapa na naamini Rais wala hatataka kusema neno atateua tu mbadala wake kwa jinsi alivyokasirika.
Dalili ya nchi kukosa amani zinaanza kujionesha nchini na dalili kuu ni viongozi wazembe na wasio wakweli ambao mara nyingi ukweli huwa hawausemi na hivyo kufanya mambo kwa kuzimazima badala ya kung'oa kiini cha tatizo hivyo kama nchi tusiyafumbie macho mambo kama haya.
Kwa kufanya hivyo ipo siku tutakuja kujuta huku tukiwa temechelewa sana!!!
Mungu ibariki Tanzania
Wasalaam.

Mauaji Tanga: Martine Shigela atumbuliwe mara moja kwa kudanganya
Poleni wana Tanga kwa kushambuliwa na magaidi yaliyowaua ndugu zetu nane akiwemo mwenyekiti wa mtaa. Sikutegemea yale ya boko halam kufanyika Tanzania lakini lawama zote ziende kwa mkuu wa mkoa na naomba atumbuliwe mara moja.
Mwezi uliopita mwanzoni waziri wa mambo ya ndani aliliambia bunge kuwa mkoani tanga kuna vikundi vya kigaidi vinavyojijenga taratibu, lakini wanajiandaa kuvisambaratisha mara moja.
Kesho yake mkuu wa mkoa wa Tanga akajitokeza mbele ya vyombo vya habari na kupinga eti hakuna vikundi vya kigaidi, anamshangaa waziri, Tanga pako salama na wananchi wasiwe na wasiwasi.
SASA hata haijapita mwezi mmoja baada ya kauli zake hizi, ndugu zetu huko tanga wameshambuliwa na magaidi hayo na kuuwawa kinyama kama kuku. Ndugu mkuu wa mkoa ulipopinga kauli ya waziri ulikuwa na malengo gani?
- Buila shaka kauli hii ya mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa tena mbele vya wanahabari ilisababisha mh waziri kusitisha mpango wake wa kuimarisha vikosi vya usalama TANGA
- Bila shaka kauli hii ya mkuu wa mkoa pia ilisababisha wananchi ku relax sana na kujisahau kuwa vigilant all time
- Bila shaka kauli hii ya mkuu wa mkoa ilisababisha hata viongozi wa usalama wa kitaifa kutotilia maanani tena kauli ya waziri kuhusu ugaidi Tanga
ulipopinga mpango wa waziri wa kuimarisha ulinzi mkoani TANGA kwa kusema eti pako salama ulikuwa na malengo yapi?
KAMA ALIVYODANGANYA ANNE KILANGO, NA WEWE PIA UMEDANGANYA, NA UONGO WAKO UMESABABISHA VIFO, HIVYO WEWE NI JIPU NA TUNAOMBA KWA HESHIMA NA TAADHIMA UTUMBULIWE.