Kwa hili hongereni CCM

MTRANSPARENT

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
740
204
Binafsi naomba kuwapongeza CCM, pamoja na kuwa sio chama changu.

Mwaka huu CCM imeonesha wazi kupambana na wagombea wanatumia pesa kununua wapiga kura walianza na Lowassa lakini vile vile kwa jimbo langu la Kibondo imenfurahisha sana kutengua ushindi wa Jamal kwani huyu mfanyabiashara anafahamika kwa tabia zake ovu ndani ya jamii lakini kanunua viongozi wa CCM wilayani na wapigakura hatimae CC imetengua uteuzi wake, pamoja na yote hili jimbo mpaka sasa ni la ACT-Wazalendo.

Kwa upande wa jimbo jirani la Kasulu hali ni hiyo hiyo mfanyabiashara ajulikanae kwa jina la Dyoya kanunua uongozi na leo tu nimekutana na uzi umeanzishwa humu JF ukimsifia Ndyoya kuwa ametenga sh.1bil kulichukua jimbo hilo lakini naye pia amekatwa nimefurahi sana na hatua hizi za CCM, jimbo hili tayari ni mali ya Machar.

Binafsi niwapongeze CCM, Lakini pamoja na juhudi zao hizo watambue wameshachelewa kule Kigoma ni upinzani tu, ndio mkoa pekee Tanganyika ambao wabunge wa upinzani ni wengi kuliko wa CCM.

Hivyo tunajitamba kuongoza harakat za mageuzi nchini.

Kwako Mkosamali umemalizwa na UKAWA jimbo ungelipata lakini kama ukishikwa mkono na Lowassa eti anakuombea kura basi ujue ndio mwisho wako Kibondo.
 
Kwani kwa Tanzania chama cha upinzani maana yake nini? Maana ACT huwa sielewi ni wapinzani wa nani? Mara watuseme ccm mara Ukawa amueni moja tuunge mkono tujue mko nasi au acha tujue hamko pamoja nasi!
 
Walioteuliwa na ccm ni pamoja na Mwigulu,ndugai, nape, - hawa wote hawakutumia pesa!
 
Hata karamagi naye imekula kwake pamoja na kutandaza senti ..chama kinaanza kutakata sasa na makapi yoote na makupe yanalifata joka kuu CCM B
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom