Faru John II
Senior Member
- Dec 27, 2016
- 134
- 135
Dr. Harrison Mwakyembe ametoa majibu alipoulizwa amefikia wapi kuhusu kuifanyia kazi ripoti ya Uchunguzi uliofanywa juu ya kinachoelezwa kuwa ni Uvamizi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam katika kituo cha habari cha Clouds Media Group (CMG).
Alipokuwa akitoa majibu Daktari huyu mwenye PhD ya sheria kama kawaida yake hakusahau kujinadi kuwa yeye ni gwiji na mkongwe ktk taaluma ya sheria ambapo hawezi kushughulika na Ripoti iliyokiuka misingi asili ya utoaji haki (RULES OF NATURAL JUSTICE). Mh. Waziri akaendelea kueleza kuwa ukitazama tu kamati ya Uchunguzi iliundwa na watu wenye interests(maslahi) na uchunguzi yaani Wanahabari pia msingi mwingine uliokiukwa kwa mujibu wake ni haki ya kusikilizwa ambapo alisema kamati yenyewe ilikiri kwa maneno yake kuwa haikuweza kumpata Mh. Mkuu wa mkoa.
KWANINI NIMEANDIKA MAKALA HII?
Jibu ni jepesi tu, Jibu lenyewe ni kuwa Rules of Natural Justice zina exceptions(ukomo). Ukomo wenyewe ni katika maeneo yafuatayo
(i)Haizingatiwi panapokuwa na haraka ya kuwepo uamuzi (emergency cases) mfano penye hati hati ya kupotea kwa amani na utulivu endapo maamuzi yatacheleweshwa.
(ii) Pale ambapo sheria haikutaja kuzingatiwa kwa misingi hiyo.
(iii) Pale ambapo kuzingatiwa kwa misingi hiyo kutahatarisha maslahi ya Umma.
(iv) Pale ambapo hatua za haraka zinahitajika
(v) Pale ambapo imeshindikana kusikilizwa kwa mtuhumiwa.
(vi) Pale ambapo mgogoro unahusiana na mambo ya kiutawala/Uongozi (purely administrative matters).
(vii) Pale ambapo hakuna haki ya mtu itapindishwa.
(viii) Pale ambapo kuzingatiwa ama kutozingatiwa kwa misingi hiyo hakutoleta tofauti yoyote katika maamuzi.
(ix) Pale ambapo mtoaji wa uamuzi hana sifa ya kuwa na kasoro.
Sheria inayoeleza sifa za watu wanaounda kamati ya Uchunguzi haijataja kuwa mwanahabari yoyote hatakiwi kuwa sehemu ya kamati ya uchunguzi, pia exceptions (vizuizi) za misingi ya asili ya haki zimeweka wazi kuwa panapotokea vikwazo vya wazi vya kutopata maelezo ya mtuhumiwa misingi hii haitozingatiwa, kamati ilieleza wazi namna Mh. Makonda alivyokuwa akikwepa kutoa maelezo kwa kuwakimbia wajumbe waliotumwa kumuhoji.
Ukitazama kwa makini maneno ya Dr. Mwakyembe kuamua kukwepa wajibu wake kisa Rules of Natural Justice utagundua kuwa kauli yake haina mashiko na haitegemewi kutoka kwa mtu mwenye elimu hafifu ya sheria. Mh. Waziri atambue kuwa kamati ile ilitazama misingi hiyo na ikatazama pia vizuizi vya kuzingatiwa kwa misingi hiyo kama nilivyotaja hapo juu ambapo ni wazi kabisa utaona issue ya Makonda ni ya kiutawala kabisa (purely administrative matter) ambapo swali lililotakiwa kujibiwa na kamati ni Je Makonda alitumia madaraka yake vibaya? Jibu la kamati likawa ni Ndio likatoa na evidence (ushahidi).
Kwa heshima na taadhima tunamwomba Mh. Mwakyembe kutuomba ladhi kwa kutufanya wajinga wa sheria.