Kwa hili ccm hatuwasamehi hata kidogo

Kwa hili ccm hatuwasamehi hata kidogo

nkongo

Member
Joined
Dec 9, 2011
Posts
84
Reaction score
14
Ccm mmejifungia dodoma kufuta vipengele muhimu vya rasimu ya katiba nasema nyinyi ccm tutawaadhibu kama sio ninyi basi watoto wenu.
mmefuta ibara ya maadili ya viongozi ili ufisadi uendelee,mmefuta ibara ya madaraka ya wananchi,mmefuta ibara inayotenganisha madaraka ya bunge na serikali.
 
wamefuta hata sura za kuenzi na kulinda utamaduni wa mtanzania badala yake wameweka kifungu cha kuwaenzi wasanii wetu wanaoshinda uchi ------ na mapaja nje
 
Kitu kikishakuwa najisi huendelea kuwa najisi. Rasimu ya warioba ilikuwa maridhawa na yenye manukato yaliyovutia taifa kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli hasa ya kumfanya mwananchi aweze kufaidi rasilimali za taifa. Ghafla wachafuzi na walafi wakaona haiwezekani fursa hii iwafikie hadi wananchi wa kawaida....wakaamua kuinajisi katiba na kupoteza harufu nzuri ya manukato yaliyovumishwa na upepo mzuuri wa wataalamu hawa wa akina jaji warioba. Kilichopo sasa walafi hawa wanalazimisha harufu mbaya iwe nzuri kitu ambacho hakiwezekani. Kutaka wajumbe wapige kura ughaibuni ni kulazimisha harufu mbaya iwe nzuri....kusema kuwa watapata 2/3 zanzibar ni kulazimisha harufu mbaya iwe nzuri. Kana kwamba wanahisi wanaanza kupata harufu nzuri linajitokeza suala lingine ambalo harufu yake ni kuu hasa kwa kuwa kuna watu wanaihisi ni nzuri na wengine wanahisi ni mbaya. Suala hili linaleta hofu kuu miongoni mwa walafi...wameanza kuweweseka watajinasua vipi mtegoni mwa kadhi (harufu kuu). Wajuvyi wa mambo walisema katiba ni maridhiano na ni dhahiri shairi walidharau maridhino awali wanayatunuku sasa hivi muda ukiwa umeyoyoma. Naomba kumalizia kwa kumnukuu Warioba kuwa "tutakutana mtaani".
 
Eee mwenyezi mungu hebu tunusuru na balaa
hili la machafuko ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom