Kwa hili busara itumike Kiteto kwa walimu

Kwa hili busara itumike Kiteto kwa walimu

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Lipo jambo lisilo la kawaida na ambalo halina tija linafanyika Kiteto, kwa kweli halistahili.

Iko hivi..Serikali ina utaratibu wa kuajiri na kupanga watumishi kulingana na ikama

Hili halina ubishi hoja hapa inawezekanaje mtu aliyesomea kitengo maalumu cha watoto wenye mahitaji maalumu kupelekwa ambako hakuna watoto hao wakati kuna kituo kimoja tu ambacho sio rasmi hakina walimu wakutosha?

Najiuliza kwa sauti kubwa tu hivi kwa walimu ambao wamesomea fani hiyo maalumu na adimu katika maeneo mengi wanajisikiaje?

Mf Wilaya ya Kiteto haina shule ya watoto wenye mahitaji maalumu na badala yake shule ya Partimbo imetengwa kuwahifadhi, pamoja na kwamba hakuna umeme, fence, walimu hawatoshi kuna sababu gani ya msingi mwalimu aliyesomea fani maslumu kupelekwa ambako hakuna hitaji hilo?

Hivi kweli ni busara kwa mtu mwenye dhamana kufanya maamuzi haya hasa katika kipindi hili cha awamu ya tano cha Rais Dr JPM?

Nadhani kuna haja ya wawaliopewa dhamana ya kumwakilisha Rais Dr John Magufuli kutupia macho suala hili kama kunahaja la kutotumia fursa kama hiyo ya mwalimu huyu kufundisha watoto hao na badala yake kupelekwa kusiko na hitaji.

Wakati mwingine uhamisho wa sampuli hii huwa ni kukomoana,...ngoje tumpeleke mahali mfali kwasababu tusimuone anatubana katika mazingira yetu.

Jamani kwamini tunafanya haya Kiteto?
 
hilo ni tatizo kweli ...nami nalijua....wale watoto bado mazingira yao hayajaandaliwa ipasavyo...pambana jamhuri
 
Back
Top Bottom