Kwa hii tabia ya wanawake ku pretend b4 marriagge tufanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hii tabia ya wanawake ku pretend b4 marriagge tufanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by feeeeez, Jul 12, 2012.

 1. f

  feeeeez Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeshuhudia mara nyingi sana kwa ndugu ana marafiki zangu wanapoamua kuoa,vile ambavyo tabia halisi ya mwanamke inakuwa imefichwa anapretend kuwa ni mnyenykevu sana,mwenye upendo ila akishaolewa na kuingia ndani ni noma. Nina nduguyangu ambaye baada ya kuoa ndipo tulipotambua kuwa shemeji yetu ni mchoyo ana ubinafsi, m2 wa maneno mengi wafanyakazi wanakimbia -hebu tusaidiane wataalamu wa saikolojia ya tabia je? kuna namna unaweza kutambua kuwa hapa m2 (mtalajiwa) anapretend tu .vilevile wawezaje kujua mwanamke mbinfsi anayepretend kuwa mwema.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wanawake wengi wenye ndoa sijui wana mapepo?
  kuna mwanamke mwingine ndani ya nyumba ukienda hupewi hata maji ya kunywa..hata karibu ya uongo..ukarimu ni ziro kabisa... huwa nashangaa sana hata mimi....
   
 3. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ni ngumu katika hali ya kawaida, labda uingie kwenye mahusiano naye ya karibu sana kwa muda mrefu au kupata taarifa indirectly kupitia watu wanaoishi naye au waliomfahamu kwa muda mrefu. Kupata taarifa kwa njia hii kuna madhara yake ikiwepo kupewa taarifa zisizo sahihi (biased), Exaggeration, na hata siri ambazo zinaweza kukukatisha tamaa ya kuendelea nae.
  Ni vizuri kuomba Mungu akuongoze kumpata mtarajiwa wa kufanana nawe kitabia, kuliko kulemea kwenye akili ya kibinadamu pekee!
   
 4. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Angalia sana hapo kwenye red, usije ukawa unatumiwa na shetani kuharibu familia ya ndugu yako!!Shauri yako
   
 5. sikafunje.N

  sikafunje.N Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi siwalaumu sana ingawaje inakera. Mwanamke anapopata full control au mamlaka anapenda aonekane kama anaweza na anajitahidi (kwa mawazo yake) kutengeneza mazingira ya kuonekana na kubana matumizi. wengi wanaamini kwamba akina baba ni wepesi kutoa.
   
 6. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tatizo watu tukiambiwa tuingie kwenye courtship kabla ya ndoa tuna waza kutoana out na kulewa na kungonoka mpaka tunasahau maana halisi ya uchumba.
  Trust me ukikaa na mtu vizuri ikupasavyo kwenye uchumba utamjua tu! hata apretend vipi, tabia sugu za mtu zitakuwa zina popup na yeye anazi suppress ukimsoma vizuri utajua tu....
  Kwa mfano kama mbeya atajisahau tu siku ataanza kukueleza habari za umbeya..
  Kama namchukia ndugu yako siku wakiwa wote utaona tu anabadilika tofauti na anavyokuwa na wewe...
  Kama mchoyo do I need to explain? Utaona tu the way anavyobehave na vitu vyake...
   
 7. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Watu wa namna hii wengi wao huwa ni maskini wa nafsi na mafukara. Mwanzo tu wa mahusiano yenu utagundua maisha anayoishi ya kimaskini ndani ya nafsi na ufukara uliokithili.
   
 8. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Tabia ya mtu hua haijifichi! Jitahidi kua nae karibu utamjua tu..tatizo lenu mnakutana leo baada ya miezi mi3 mnaoana what do you expect??
   
 9. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hizo ndoa za milele ndio shida yake hiyo. Dawa ni kupiga chini tu hakuna haja ya kuvumiliana. Maisha hayaji mara mbili. Ndio maana ya "We live only once !!!"
   
 10. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Da utafikiri umemUona wifi yangu .Kla sentence uliyoandika yani ni yeye tabia zake umepesti hapa kabla hayaolewa tulijua tumepata wifi.lakini do ndani ya mwaka.hata mguu nimekata wa kwenda kwake wafanyakazi ndo usiseme maneno machafu hata kwa mumewe.Da i feel pity for my brother he is so good.
   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kama unakubali kuwa tabia kwa asilimia kubwa inatokana na malezi...ukitaka kujua tabia ya mkeo mtarajiwa chunguza tabia ya mama yake. Fuatilia kwa majirani zao uliza mama mkwe ana tabia gani...simpo

  Nakumbuka mama yangu alimkataza kaka yangu aimwoe dada fulani kwa kuwa kwao though kulikuwa mbali kidogo na kwetu tulikuwa tunapajua na mama alikuwa anamjua mama mzaa chema nje ndani...Mama yake huyu mdada alikuwa na sifa ya kumweka mumewe kiganjani; afurukuti; na ni mke wa kati kati ya wake watatu...hivyo mama yangu alikuwa anasema mama wa huyu dada lazima atakuwa keshamfundisha mwanawe ushirikina.Lol. Hivyo kaka akioa nae asubiri kutengenezwa.


   
 12. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mtoto akikulia mazingira ya mama mchoyo naye atakuwa mchoyo.

  Juzi kati nilikuwa nasoma article moja kuhusu tamaduni za wasukuma...imeandikwa na scholar wa nje kwenye journal kubwa tu kama nakumbuka ni ya Cambridge...huyo jamaa amefanya ethnograph usukumani anasema wasukuma wanawaforce watoto wao ku share chakula na majirani ndio maana ni kabila ambalo ni most generous in Tz.

  Kama ukarimu ni kigezo kikubwa kwa mke umtakaye...nakushauri ukaoe usukumani. Lol.
   
 13. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Kumbe hata karne hii kuna watu wanaamini haya mambo.

  Duh aijuaye mvua imemnyea, na ajuaye ushirikina kuna uwezekano mkubwa kashiriki.

  Anyway, asante kwa kujuza.
   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kama wewe huna hiyo imani kinachokufanya ushukuru ni nini?

  Ushirikina upo na kuna watu wana mpaka PhD za research ya mambo ya giza Afika; tena ni wazungu.

   
 15. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  kujuza kwamba na wewe ni muumini wa mambo hayo kutokana na mazingira lol. Salamu kwa shemeji.
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hivi kujua kuwa kuna watu ni waumini wa Freemason lazima na wewe uwe? Angalia maandishi yako binti. Mimi ni NK kama hunifahamu vizuri. Niko juu na hakuna wa kunishusha... hata uni provoke vipi.
  Nina experience na watu kama nyie na wengi wamejaribu wakaishia kushuka wao.

   
 17. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  bwa ha ha haaa. Bahati mbaya siko hapa kufahamu mtu, aliyepanda wala kushuka, aliye juu wala chini.

  Ushikwapo shikama na ukizidiwa poa.
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,700
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Kuwepo na pre-marriage!
   
 19. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hyo sawa kabisa, au pawe na probation..............lol
   
 20. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaan nakubali maneno yako,, yaan mtu anaficha makucha yake mpka pale keshaingia ktk ndoa ndio unajua.kuwa si paka kumbe chui
   
Loading...