Udini, Elimu na Mabaraza ya Katiba Mpya (Ngazi ya Wilaya Mamlaka ya Serikali za Mitaa)
Nianze na udini Taifa kwa sasa liko katika hali ya kunyoosheana vidole kati ya dini kuu mbili Wakristo na Waislam kutokana na matukukio yanayoendelea hivi sasa. Ebu jiulize hivi sisi wananchi wa kawaida mitaani kwetu tunakoishi tunabaguana kwa misingi ya kidini? Kuna chuki kweli kati yetu? Jibu lake ni hapana.
Wanasiasa hasa chama tawala si mara moja wamesimama kwenye majukwaa wakiwatahadharisha wananchi kutokuwasikiliza na kuwaunga mkono wapinzani kwa sababu ni wadini wakianza na CUF(Uislam) na sasa CHADEMA(Ukristo) lengo kuu ni kuua nguvu ya vyama hivi vinapo onekana tishio kwa chama tawala. Ndio maana leo CUF aizungumziwi tena kama chama cha udini bali CHADEMA kwa sababu ndicho chama kikuu cha upinzani kwa sasa.
Kauli hizi zimekuwa zikitolewa hadharani na viongozi waandamizi wa chama na serikali bila kificho. Katika uchaguzi mkuu wa 2005 CUF waliitwa wadini kisa tu viongozi wake Waandamizi wengi walikuwa Waislam na kilikuwa na nguvu Zanzibar ambako wanachi wengi ni waislam.
2010 CHADEMA kikaitwa chama cha wakristo tena wakatoliki kwa kuwa katibu wake Mkuu akiwa mgombea uraisi ni mkristo mkatoliki aliyewai kuwa Padri. Sikuwai sikia popote pale katika uchaguzi ule kiongozi wa CHADEMA akisema msichague CCM kwa sababu ya udini bali ilikua ufisadi, rushwa, umaskini nk.
Kauli hizi za udini zikawafikia waumini wa dini hizi, Wakristo hasa Wakatoliki wakaanza kuona kama vile wanabaguliwa na Waislam nao wakaona kumbe nasi tumpe wa kwetu rais Kikwete. Tofauti hizi zikaanza kuwafanya waumini wa pande zote mbili kudadisi nani anashika wadhifa gani kwa kuangalia dini yake wakati na baada ya uchaguzi.
Mpasuko huu uliendelea kuzaa tofauti za kidini mpaka kupelekea Sensa ya makazi na watu 2012 kutaka kususiwa na upande mmoja wa dini hizi kuu mbili. Cha kusikitisha kauli zile za CHADEMA ni wadini zinazotolewa na CCM hazikukemewa wala kusitishwa zinaendelea mpaka leo. Madhara yake sasa ni kujenga mijadala mingi ya kidini iliyo amsha isia nyingi zilizotupelekea hapa tulipo leo.
Kauli zinazotolewa hazilengi kumaliza tatizo bali zinazidi kulikuza kwani CCM na Serikali hawawazui watu wao kuendelea kukiita CHADEMA chama cha kikristo, hili hali CHADEMA hawajasema hata mara moja CCM ni chama cha kidini nje ya ufisadi, rushwa, umaskini nk.
Rais Kikwete toa kauli zuia watu wako kuviita vyama vya upinzani ni vya udini hili hali havijawai kuhubiri udini majukwaani. Si sahihi kuendeleza propaganda hizi za udini dhidi ya CHADEMA hili hali chama akina sera wala itikadi za udini japo Viongozi wake wana dini, wanachama na wapenzi wake wana dini kama ilivyo kwa CCM.
Haya ndio madhara ya kusingizia udini matokeo yake ndio haya taifa linaelekea kumeguka shauri ya upumbavu wa CCM wa kuubiri udini kwenye majukwaa ya siasa. Pili kuna bomu lingine linatengenezwa na CCM kama hili la udini nalo ni ukanda na ukabila likilipuka tusianze kuulizana mchawi ni nani, CHADEMA kiko Tanzania nzima kina viti vya ubunge kaskazini, magharibi, kati, na nyanda za juu kusini. Hata huko kilimnajaro na Arusha CCM ina majimbo mengi kuliko CHADEMA.
CCM acheni mara moja kuyatamka haya hadharani ili hali takwimu zinakinzana na mnachokisema, kesho uchochezi huu ukikolea kwa wananchi ni hatari kwa umoja wa taifa letu.
Kwa leo naomba niwasilishe la udini pekee yaliyobaki ntayaleta kwenu kadri Mungu atakavyozidi kutupa nguvu na uzima.