Jana, Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemtimua uanachama wake, muasisi wa chama hicho na Muungano, Mzee Hassan Nassoro Moyo kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi yasiyokubalika na sera za chama chao.
Ni Majuzi tu, CCM walikuwa wanasema Zitto anaonewa kwa kujifukuza uanachama wake kupeleka masuala ya chama Mahakamani, na kuweka pingamizi asijadiliwe kwa kuanzisha chama cha ACT akiwa chadema. CCM kama mnapenda Wasaliti wasifukuzwe kama alivyofanyiwa Zitto na chama chake, mmemfukuzaje Moyo?? kwa hiyo wanaokiuka kanuni za vyama vingine wabaki ila wanaokiuka kwenu wafukuzwe.
Kila kitu nyie. Shaaban Robert akiandika mashairi wakati wa Ukoloni alihoji "Kwao kwao kwanini na kwetu kwao kwanini" CCM mnataka kuendesha chama chenu na vyama vya upinzani muendeshe kwanini???