Navyojua mimi kuupandisha mji hadhi na kuitwa jiji kuna mengi yakuzingatia na ya kuangalia
Kwa hapa Arusha me nadhani bado hatujikidhi kuitwa jiji, mfano miundo mbinu,usafi,mipango mji
Rais anakuja na misafara mikubwa kufungua jiji la Arusha wakati mitaro michafu hata hapo stadium anapokuja hutubia chemba za maji taka zimepasuka kunanuka,mitaro imejaa kuchafu wa kila aina kuzunguka mji,
barabara nyembamba magari hayapishani
Madampo ya uchafu hakuna kila mahali kuna majalala yasiyo rasmi uchafu umetapakaa kila kona
usanifu wa majengo nao ni tatizo japokua kuna wingi wa gorofa zinajengwa lakini bado hazijawekwa kwenye mpangilio mzuri(holela)
machinga hawajapewa eneo ambalo litawakidhi na wataendana nalo kwa biashara zao
maji nayo ni tatizo kwa mitaa mingi ya arusha
hali ya kisiasa pia bado sio shwari hatma ya umeya kwa pande zote mbili bado ni tete
kuna mengi yanafanya mji wa arusha ujizatiti kwanza ndo upewe hadhi ya JIJI