Kwa anayeifahamu Mwenge Catholic University

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,910
Reaction score
18,558
Nataka kufahamu kuhusu upatikanaji wa malazi (accommodation) kwa wanafunzi wa Mwenge Catholic University huko Moshi.

Je, chuo kina nafasi kiasi gani kwa ajili ya malazi ya wanafunzi na kwa gharama ipi?

Je, kwa accommodation nje ya chuo upatikanaji wake ukoje na kwa gharama ipi?
 
Mkuu umepangiwa hapo?

ndani ya chuo ni 250,000/ kwa mwaka. nje ya chuo vyuo ni kuanzia 40,000/- , na nje unakuja chuo kwa miguu hamna nauli kama ilivyokawaida nyumba zakupanga zimejengwa karibu sana na chuo.

Hostels zinapatikana japo wengi hupenda kukaa nje, karibu!
 
Karibu sana mkuu,kuna vyumba mpaka elfu 25 ila ujue kutembea maana ni mbali na chuo,vyumba vya karibu be elfu 40 mpaka 70.Hostel mkuu kakupa jibu hapo juu,chakula kuanzia buku mpaka 1300,hicho cha buku full amira jiandae na kuzalisha gesi.Siasa ziache nyumbani kwenu na nguo za ajabu haswa kama wewe ni ke,kama una kitambi usijali kitaisha chenyewe maana ni seminary hapo unapoelekea.Karibu Rumi mkuu.Shule ipo mpaka uombe poo.
 
Mkuu,usisahau kuja rainboot Moshi tope lake ni shida,hii michina tunayovaa utanunua kila ijumaa.Kuna swali lingine mkuu?karibu sana Rumi.
 
mkuuu umenichekesha sana eti kitambi kitaisha.
nlivyoanzaga mwecau nlikuja chuo nmechelewa kama mwezi na wiki hivi, bwana we kidogo nichizikeeee lecture rooms cjazijua vizur ile unaijua tu leo kesho nakutana na test, yaaaan yaaaan
 
umemkumbusha jambo jema nguo za ajabuajabu atavaa weekend getini hatopita
 
mkuu umepangiwa hapo?? ndani ya chuo ni 250,000/ kwa mwaka. nje ya chuo vyuo ni kuanzia 40,000/- , na nje unakuja chuo kwa miguu hamna nauli kama ilivyokawaida nyumba zakupanga zimejengwa karibu sana na chuo. hostels zinapatikana japo wengi hupenda kukaa nje. karibu

Nashukuru sana kwa majibu niliyohitaji. Kuna mwanangu amechagua kuja hapo hivyo nimeona nianze mapema kuifahamu shule na mazingira yake ili nijipange kumhudumia vizuri.
Hiyo gharama ya nje 40,000/ nadhani ni kwa mwezi, na wenye Nyumba wanahitaji ulipie kwa miezi mingapi? Je wanaweza kukubali kulipia mwezi mmoja mmoja?
 
wengi wanapenda miezi 6, chakula ni kuanzia 1000(japo hata shiba) hadi 1500 afadhali
 
Hiyo nimeipenda! Imenifanya nikipende chuo!

yaan MWECAU suruali, vinguo vifupi kupita magoti, zinazoonyesha(transparent), sijui mlegezo mwambie abebe chache maana atavaa nje ya chuo tu maana mlinzi hakubali upite akikupitisha ukakamatwa ndani ya chuo unarudishwa geti ulopitia mlinzi inakula kwake
 
Karibu sana mkuu,kuna vyumba mpaka elfu 25 ila ujue kutembea maana ni mbali na chuo,vyumba vya karibu be elfu 40 mpaka 70.Hostel mkuu kakupa jibu hapo juu,chakula kuanzia buku mpaka 1300,hicho cha buku full amira jiandae na kuzalisha gesi.Siasa ziache nyumbani kwenu na nguo za ajabu haswa kama wewe ni ke,kama una kitambi usijali kitaisha chenyewe maana ni seminary hapo unapoelekea.Karibu Rumi mkuu.Shule ipo mpaka uombe poo.

Kwa kweli umenifanya nikipende chuo hiki! Taratibu hizo nazipenda sana, nguo za ajabu ajabu za nini? Hapo kwenye kutembea je kwa wastani ni kilometa ngapi unatembea kwenda chuoni?
Je kwa first year ipi bora, kukaa ndani ya chuo au kupanga nje ya chuo?
 
yaan MWECAU suruali, vinguo vifupi kupita magoti, zinazoonyesha(transparent), sijui mlegezo mwambie abebe chache maana atavaa nje ya chuo tu maana mlinzi hakubali upite akikupitisha ukakamatwa ndani ya chuo unarudishwa geti ulopitia mlinzi inakula kwake

Kwangu mimi kama mzazi hiyo ni safi sana! Nguo fupi za nini? akizihitaji atazivaa akiwa chumbani kwake!
 
wengi wanapenda miezi 6, chakula ni kuanzia 1000(japo hata shiba) hadi 1500 afadhali

Na hicho chumba anakuwa peke yake au wanakuwepo na wengine na kila MTU anatoa 40,000/= au wote mnaokaa chumba kimoja mnachanga ili zifike 40,000/=. Kwa maneno mengine ni sh.40,000/= kwa chumba au kwa kichwa kimoja?
 
chumba cha 40 au60,50 ni kwa chumba sio kichwa mkikaa 2 mfano kodi ni 50/60 (kwa self) mnatoa nusu nusu ili ifike hiyo
 
Back
Top Bottom