Kwa anavyodhalilishwa na Kikwete, ungemshauri nini waziri mkuu Mizengo Pinda?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
003.KIKWETE.JPG

gado.jpg


Kwa wanaojua jinsi waziri mkuu Mizengo Pinda anavyotumika kama nepi au tuseme zimamoto na rais Jakaya Kikwete, wanamuonea huruma. Je ni kwanini yeye hajionei huruma akaachia ngazi? Au anahitaji ushauri nasaha. Je wewe ungemshauri nini Pinda ili angalau ajiwekee legacy yenye kueleweka?
 
Kondoo wa kafara huyo, wacha afanywe hivyo hivyo, anapenda na kukubali kwa moyo mweupe.
 
Pinda boi si boi wala mtumwa si mtumwa, yupo yupo tu kulinda muda utakapofika aomdoke nae ajulikane kama alikuwa waziri mkuu basi; lakini zaidi ya hapo jamaa anatumiwa na mkweree kama janvi tu!! Kusema kweli Pinda anahitaji ushauri nasaa kwani tabia yake sio ya kawaida.
 
Pinda is beyond redemption hata kujiuzulu haisaidii...the damage is too great kwa sifa yake na hata kwa muktadha wa nchi yetu. Njia bora ni kufuata mfano wa wajapani wa zamani i.e. to commit Seppukku yaani atafute kamba aende pale mnazi mmoja kwenye uwanja wa mashujaa na ajitundike na kujinyonga. hiyo ndio njia pekee ya kujikosha aibu yake na watu labda wataanza kumwelewa na kumsamehe kwa usaliti wake na anaweza kuitwa shujaa wa kuwajibika!
 
sina cha kumshauri kwani ataanza kulia, na mimi sio mzuri kwenye kubembeleza
 
Pinda is beyond redemption hata kujiuzulu haisaidii...the damage is too great kwa sifa yake na hata kwa muktadha wa nchi yetu. Njia bora ni kufuata mfano wa wajapani wa zamani i.e. to commit Seppukku yaani atafute kamba aende pale mnazi mmoja kwenye uwanja wa mashujaa na ajitundike na kujinyonga. hiyo ndio njia pekee ya kujikosha aibu yake na watu labda wataanza kumwelewa na kumsamehe kwa usaliti wake na anaweza kuitwa shujaa wa kuwajibika!

No comment. Huyu mzee mimi nilitokea kumpenda ghafla, mpaka leo hii naendelea kumpenda tu regardless amefanya nini. Tatizo la system ya "uongozwa" wa watanzania haukinzani na viongozi wenye roho nzuri na maadili mazuri, simply mi nadhani tunaoongozwa hatuko hivyo ndiyo maana hatuwezi ku-cope na viongozi wa namna hiyo, except wenye roho mbaya, mabavu na ufisadi! Matatizo ya viongozi wetu wengi (ukimuondoa Waziri Mkuu na baadhi of course), yana-reflect namna sisi waongozwa tulivyo!
 
Jenerali Ulimwengu

236
25 Apr 2012

NCHI inapitia kipindi tete, kipindi ambacho kinashuhudia maswali mengi yakiruka kutoka kila upande huku kukiwa hakuna majibu yanayoeleweka. Halitakuwa kosa kuieleza hali hii kama hali ya mkanganyiko wa kitaifa.

Hivi majuzi niliandika makala katika mlolongo wa safu hii iliyosema kwamba “kupotea tulikopotea ni kupotea kukubwa.” Hali tuliyo nayo leo hainipi sababu ya kudhani kwamba hali yetu ya upotevu imebadilika sana, isipokuwa tu kwamba watu wengi zaidi wametambua kupotea kwetu ama wameamua kukupigia ukunga, kusema kwamba hata wao wameuona upotevu huo.

Hivi majuzi Rais Jakaya Kiwete ameiapisha tume yake aliyoiteua kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Napenda kuwapa pole wote walioteuliwa kwa kubebeshwa mzigo usiobebeka, kwa sababu ambazo nitazieleza leo na katika makala nyingine zijazo.

Kimsingi, ninachokiona mimi ( na wala siko peke yangu katika hili) ni kwamba tuko katika hali ya wananchi kufurukuta wakitaka mabadiliko makubwa yafanyike na yaonekane yakifanyika, lakini wakikabiliana na utawala uliokufa ganzi na kuduwaa, usijue la kufanya. Wananchi wanaumia, wanahenya, wanalalama, wanatafuta majibu, lakini wanakutana na maswali zaidi.

Kila mtu anajua kwamba hali ya maisha kiuchumi imekuwa ngumu sana, hususan katika maisha ya watu wa kawaida ambao wanaathirika vibaya kutokana na gharama za maisha kuzidi kupanda kutokana na bei za mafuta na chakula kupanda kila uchao. Hawaoni jitihada zo zote za serikali yao kupambana na hali hiyo, na badala yake wanashuhudia wakubwa ndani ya serikali wakizidi kujijengea ukwasi usiokuwa na maelezo.

Taratibu, wananchi wameanza kutambua kwamba ufukara wao katika mazingira ya nchi tajiri sana unahusiana moja kwa moja na utajiri mkubwa wa watawala wao ambao wamekuwa wakitumia ofisi zao kujikusanyia mali haramu. Ofisi za serikali sasa zinajulikana kuwa ni mali binafsi za wale waliowekwa mle eti kuwatumikia wananchi. Kila anayepata nafasi hiyo ameiona kama ‘kihamba’ chake binafsi bila kujali maslahi ya nchi.

Jambo moja linajidhihirisha kila mwaka, nalo ni kwamba kila siku uozo wa watawala wetu unazidi kujidhihirisha kwa kiasi kile kile ambacho tunadhihirisha udhaifu wa jamii yetu kukabiliana nao.

Kwa mfano, ofisi ya CAG ina maana gani kama kila mwaka inatoa taarifa inayoonyesha ubadhirifu katika idara za serikali lakini hakuna hatua yo yote inayochukuliwa kutokana na taarifa hizo?

Hakuna shaka kwamba ofisi ya CAG inaendeshwa kwa gharama kubwa na ziara za uchunguzi zinazofanywa na ofisi hiyo ndani na nje ya nchi ni mzigo mkubwa kwa bajeti ya nchi, na gharama hizi hatimaye zinabebwa na mlipa kodi. Kama tunajua kwamba taarifa za CAG hazina umuhimu kwa sababu hakuna dhamira ya kuzifanyia kazi, ni kwa nini ofisi hiyo isifungwe ili, angalau, tupunguze matumizi katika eneo hilo finyu?

Ofisi ya CAG ni kielelezo cha undumilakuwili wa utawala wetu. Sipati neon toshelezi la kuielezea hali hii, hivyo nalazimika kutumia neno la Kiingereza ‘schizophrenia,’ kwa maana ya kuwa na hulka mbili kwa wakati mmoja.

Kwa upande mmoja, tumerithi kutoka kwa wakoloni vyombo vya udhibiti ambavyo kazi yake ni kuhakikisha kwamba fedha za serikali hazitumiki hovyo, na kwamba pale zinapothibitika kutumika hovyo, wahusika wanachukuliwa hatua.

Lakini kwa upuuzi wetu hatuna dhamira ya kuchukua hatua pale inapobidi kwa sababu, kimsingi, ni kama tumekubaliana kwamba kila mtu atajinufaisha na ofisi yake, na kwa hiyo hakuna wa kumsema mwenzie.

Kwa maana hiyo, ingekuwa hatua ya mantiki kuifutilia mbali ofisi ya CAG, lakini hiyo ingetusababishia matatizo na wafadhili ambao wangetusuta kwa kufuta ofisi muhimu kama hiyo.

Hivyo, basi, tunayo ofisi ya CAG ambayo inatoa taarifa za kila mwaka ambazo hazifanyiwi kazi lakini hatuifuti kwa sababu wafadhili watatusuta. Watu wa ajabu!

Kuna jambo ambalo inawezekana watawala wetu wamekosa kuliona kutokana na ulafi wao na uwezo mdogo wa kufikiri unaotokana na ulafi huo. Kuruhusu ofisi ya CAG kutoa taarifa hizi kila mwaka zikionyesha wizi mkubwa wa fedha za wananchi bila kuzichukulia hatua ni njia mojawapo ya kujenga chuki ya wananchi dhidi ya serikali. Serikali inayofikiri ingechagua moja: ama kuzifanyia kazi taarifa hizo, ama kuzipiga marufuku kabisa na kuifuta ofisi ya CAG. Kwa sasa serikali yetu ni ‘schizophrenic.’

Kwangu mimi ni dhahiri kwamba siku wananchi watakapochukua hatua ya kuwaadabisha watawala wao, hoja mojawapo itakayowasukuma itakuwa ni taarifa za CAG zisizofanyiwa kazi.

Wiki iliyopita, bungeni, tumepata ushahidi mwingine kwamba watawala wetu wameshindwa kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya. Baadhi yao wamebanwa na wabunge ambao bila shaka wamesukumwa na hasira za wananchi dhidi ya utawala wa ubadhirifu, wizi, kutokujali, na upuuzi. Katika sakata tulilolishuhudia bungeni, mojawapo ya sababu za malumbano yale ni taarifa za ubadhirifu serikalini (kutoka kwa CAG na kwingineko) ambazo serikali inaonekana kutokuwa na uwezo wa kuzishughulikia.

Kusema kweli, sura iliyojitokeza wiki hii iliyopita ni kwamba hatuna serikali inayofanya kazi kama serikali, bali tuna mkusanyiko wa maofisa waliokabidhiwa ofisi mbalimbali ambazo wanazitumia kadri wanavyojua wao na wala hawana udhibiti wa kati (central control).

Kila mmoja anasema anavyotaka, na katika kusema huko tunagundua kwamba katika ofisi yake anatenda anavyotaka pia, na hana ofisa mwandamizi wa kumwelekeza.

Walichotuonyesha watawala wetu wiki iliyopita ni taswira ya mkanganyiko mkubwa na wa kutia wasiwasi kwa ye yote anayethubutu kufikiri kidogo. Nchi hii haijakabiliwa na janga kubwa la ghafla katika miaka ya karibuni. Hatujakabiliwa na vita, mafuriko makubwa wala milipuko mikubwa ya magonjwa ya kutisha. Tuthubutu kujiuliza, je, iwapo tungekabiliwa na mojawapo ya majanga kama hayo, wale tuliowaona na kuwasikia bungeni Dodoma ndio tungewaamini kwamba wangetuongoza kuishinda dharura hiyo? Wale?

Nasema hapana. Tulichokishuhudia ni msamabaratiko ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii, serikali iliyoparaganyika, mawaziri wenye kauli za kitoto, wakuu wa serikali wasiokuwa na maamuzi, waziri mkuu kivuli asiyekuwa waziri mkuu, na mkuu wa nchi mtoro.

Hapo juu nimewapa pole wale walioteuliwa katika tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hii ni kwa sababu namheshimu sana Joseph Warioba, kama ninavyowaheshimu baadhi ya wajumbe wa tume yake. Ningependa Warioba, ambaye tunajua sote ni mtu makini, afanikiwe nasi tupate manufaa.

Katika wiki zijazo nitaieleza ‘pole’ yangu, lakini nianze tu kwa kusema kwamba, katika kazi ambazo zinaweza kufanywa na tume hiyo katika muda mfupi iliyopewa ni kuangalia nafasi ya waziri mkuu asiye waziri mkuu, anayefanya kazi chini ya mkuu wa nchi asiyekuwapo, na anayewasimamia mawaziri asiowasimamia na wanaofanya shughuli zao binafsi.

Hivi tunaelezaje kwamba inafikia hatua ya wabunge (bila kujali vyama) wanachukua uamuzi wa kufanya jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia yetu, kama kusukuma hoja ya kutokuwa na imani na serikali kwa sababu mawaziri wachache wanaoonekana wameboronga hawataki kuondoka hata pale wanapotakiwa kufanya hivyo na chama chao bungeni, halafu waziri mkuu hana kauli na bosi wake yuko ughaibuni?

Kama nilivyosema kuhusu ofisi ya CAG asiye CAG, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri mkuu asiye waziri mkuu? Niliwahi kuijadili mada hii katika safu hii yapata miaka miwili iliyopita, nikieleza ‘schizophrenia’ ya ofisi hii.

Nilieleza kwamba katika mojawapo ya mazoezi ya kuunda serikali katika miaka ya sabini, Mwalimu Nyerere alimteua Edward Sokoine kuwa waziri mkuu, na akaulizwa na waandishi wa habari kwa nini anamteua waziri mkuu wakati Katiba haitaji ofisi hiyo.

Jibu la Mwalimu lilikuwa ni kwamba, kweli, Katiba haikusema kwamba kutakuwa na waziri mkuu, lakini pia Katiba haikutamka kwamba hakutakuwa na waziri mkuu, na kwamba waziri mkuu ni waziri kama mawaziri wengine isipokuwa yeye yuko kidogo juu ya wenziwe. ‘Schizophrenia.’

Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa “shughuli za serikali bungeni” lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu.

Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga “Shut up!,” hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.
 
Back
Top Bottom