Wajinga bado wapo.
Hii ni story ya kweli kabisa nimesimuliwa na mtu maskani. Ipo hivi kuna boda boda alipigiwa simu na namba ngeni.
Namba ngeni: Xx aloo
Boda boda: Haloo niaje
Namba ngeni: Eh bhana ww ni boda boda ? Nahitaji sahani kumi za wali nipo mangamba day hapa nichukulie ukija utachukua hela yako
Boda boda: Ebhana sikujui namba ngeni nani mwenzangu?
Namba ngeni: Chukua wali sahani 10 kama kuna mgahawa karibu njoo Mangamba day utapewa hela yako shida nini?
Kutoka bodaboda alipo na Mangamba day ni mwendo wa dakika kadhaa tu hata dakika 5 hazizidi, kwa wanaokujua Mtwara wataelewa.
Boda kaenda hadi kwenye mgahawa jamani kuna namba ngeni imenipigia inataka wali plates 10 lakini mimi simjui kwa hiyo uamuzi ni wenu.
Mama ntilie akaona haina shida mteja wa haraka huyu akapakua sahani kumi na kuziset tayari kwa safari
Maraaa riiing hapo tayari tapeli yule kashapata namba ya mama ntilie anampigia na kumwambia ongeza na soda 10 bill yako utaikuta huku.
Boda na mama ntilie hao dukani kuchukua soda ila kabla hawachukua soda tapeli anapiga tena, soda achana nazo naomba utumie kiasi flani kwenye simu tununue luku umeme?
Je, kiasi gani 57,000 ? Tapeli anasema 57,000 jamaa wakatuma 57,000 wao hope yao si wanapelekeka shule chakula na maeneo hayo wakajua labda ni walimu kwa hiyo hela ipo tu lakini hakuna ubabaifu.
Jamaa katoka na pikipiki hadi Mangamba day na sahani zake za wali kufika anapiga simu kwa wahuni walioagiza chakula lakini ikawa simu haipokelewi. Piga sana simu hazipokelewi mwisho wa siku ikawa simu haipatikani kabisa.
Jamaa kurudi kwenye mgahawa pale kuelezea situation ilivyokuwa basi tena ndio ikawa hivyo. Shida ikaja dukani kule alietuma hela anasubiri hela yake aliyotuma mbona haletewi?
Wakamueleza kuwa tumetapeliwa sijui hivi na vile, akawaambia msiniletee ujinga sasa nyie si ndio mmetapeliwa mimi nataka hela yangu sitaki kusikia kuhusu chochote.
Huku na huku basi hela ikabidi ilipwe na mama ntilie. Sasa mama ntilie analalamika kama bodaboda kawauza kwamba yeye ndio mchora ramani.
Je, bodaboda ana makosa kwa kumuamini namba ngeni, au alitakiwa kumpuuza?