Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,182
- 2,014
Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ibara ya 3(1) inatamka kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, na ikatungiwa sheria namba 4 ya mwaka 1992, ibara ya 5, na sheria ya 2005 namba 1 ibara ya 4, yote hyo kutia uzito mfumo wa vyama vingi na demokrasia ya vyama vingi.
Na kule Zanzibar katiba yao ya mwaka 1984 iliyoboreshwa ktk toleo la mwaka 2010 imetamka ktk ibara ya 5 kuwa Zanzibar itafuata mfumo wa vyama vingi na ikatungiwa sheria namba 2 ya mwaka 2002, kifungu cha 3 kikieleza juu ya demokrasia ya vyama vingi.
Je kitendo cha rais magufuli kupiga marufuku shughuli za siasa huku CCM wakiahidi kufanya, na vyama vya upinzani wakizuiwa kina tafsiri gani?
1. Je rais amevunja katiba au hajaeleweka?
2. Leo tar.25/06/2016 alikuwa anatoa agizo kwa jeshi la polisi sambamba na kuwapongeza kwa kuzuia demokrasia ya siasa, je alikuwa na maana hiyo?
3. Urais ni cheo cha mwisho na ndo mkuu wa nchi. Je rais alikuwa ana maana sawa kama wanavyodai wapinzani?