Kuyumba kwa Uchumi: Kampuni ya Mwananchi kupunguza wafanyakazi baada ya mapato kushuka

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Wakuu,

Hali ni mbaya. Tunaweza kuchukulia poa lakini watanzania ndo wanapoteza ajira hivyo!

0a57fe9a16a59a3d48e4d88f5c1dcb62.jpg
 
Watasema walikuwa wapiga dili ndiyo maana wana hali mbaya, hii ndiyo Serikali ya viwanda
 
Vi-wonder vinazidi kuongezeka, naona TBC haina dalili ya kupunguza au yenyewe bado ruzuku ipo ya kutosha
 
Pole sana kwa wafanyakazi, nafikiri na serikalini muda siyo mrefu panga litapita.
Mkuu serekali imepunguza vya kutosha kupitia watumishi hewa, vyeti feki. Ni balaa, we sikia tu kwa mwenzio
 
Watumishi wa serikali tujipange kupigwa lidandasi kiukweli hali mbaya huku maofisini hasa huku halmashauri ni aibu wakuu wa idara hata hawajui cha kufanya ofisi zimedoroka haijawahi tokea kwa trend hii ya uchumi watumishi serikalini tusijeshangaa kupigwa lidanda wakati wowote kiukweli serikali inatembelea rim matairi hayana upepo yanakanyagiwa hivyohivyo na dereva hanampango wa kupunguza spidi na anazidi kuongeza mzigo
 
Back
Top Bottom