Kuyeko atimiza ahadi ya kulipa ada ya shule kwa mtoto wa Anderson

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Leo tarehe 15/06/2016 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko ametimiza ahadi yake ya Tshs.1,000,000 kwa Mtoto wa Marehemu Anderson Rweyemamu ambaye alikuwa Katibu wa baraza LA vijana la Chadema-Bavicha Jimbo LA Segerea.

Mhe. Kuyeko aliahidi kutoa kiasi hicho cha pesa mnamo tarehe 17/05/2016 wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Anderson lengo ikiwa ni kulipa ada ya shule ya mtoto. Mhe. Kuyeko amekabidhi kiasi hicho cha fedha kwa mama wa Mtoto Mbele ya Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe. Omary Kumbilamoto, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea Kamanda Gango Kidera.

Katika kutimiza zoezi hilo Mhe. Kuyeko amemshukru Mwenyezi Mungu kwa kumuongoza kutimiza ahadi hiyo kama alivyoahidi na amemtaka mama wa Mtoto huyo (mke wa marehemu Anderson) kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kulipa ada ya shule ya mtoto.

Aidha, Mhe. Kuyeko amemtumia salaam za pongezi Mhe. Waitara Mwita mbunge wa Ukonga kwa kushinda Kesi ya Uchaguzi iliyofunguliwa dhidi yake na aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM kwa Jimbo hilo ndugu Jerry Silaa. Mhe. Kuyeko amesema mahakamani imetenda haki kwa watu wa Ukonga na sasa mbunge wao atafanyakazi ya kuwahudumia wapiga kura wake na taifa kwa Amani na utulivu.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea Kamanda Gango Kidera amempongeza Kuyeko kwa kutimiza ahadi hiyo kwa mtoto wa marehemu. Kidera amemwambia Mhe. Kuyeko kuwa ni miongoni mwa viongozi wa chache wanaoweza kutimiza ahadi zao, hasa kwenye maswala ya kijamii.

Katika kutimiza ahadi zake Mhe. Kuyeko pia ametimiza ahadi yake ya kulipia ofisi ya Chadema ya Kata ya Bonyokwa na ofisi zote za Chadema katika matawi yaliyoko Kata ya Bonyokwa. Zoezi hilo amelifanya kwa lengo la kusaidia ujenzi wa Chama ndani ya Kata ya Bonyokwa.

Mhe. Kuyeko na Kamanda Kidera kwa pamoja wametoa rai kwa viongozi wote wa kiserikali wanaotokana na Chadema watumie nafasi zao kusaidia kukijenga Chama hasa swala la ofisi. Kamanda Kidera amemwambia Mhe. Kuyeko kuwa umeonyesha njia katika kukisapoti chama naamini Madiwani wenzako nao wataiga mfano wako kwa Kata zao.

Imetolewa Leo 13/06/2016
Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.
0656-568256
 

Attachments

  • IMG-20160615-WA0068.jpg
    IMG-20160615-WA0068.jpg
    46.3 KB · Views: 38
  • IMG-20160615-WA0070.jpg
    IMG-20160615-WA0070.jpg
    34.2 KB · Views: 43
  • IMG-20160615-WA0069.jpg
    IMG-20160615-WA0069.jpg
    28.6 KB · Views: 40
Back
Top Bottom