Kuwepo kwa BASATA na MWENGE WA UHURU ni ishara ya matumizi mabaya ya pesa za umma

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Wakati viongozi wanajinadi kubana matumi yasiyo ya lazima, inashangaza kuona taifa lina mambo na vyomba vya hasara vingi vikiendelea kulitia taifa hasara zisizoeleka!

Baadhi yake ni baraza la sanaa la taifa, BASATA, NA MWENGE WA UHURU ambao mpaka dakika hii unaendelea kulitia hasara taifa LIVE! Huku TBC ikikosa pesa za kurusha LIVE matangazo ya Bunge.

Kwa upande wake BASATA haijawahi kuwa na faida yoyote kwa taifa zaidi ya kulitia taifa hili hasara za kila namna. Naisihi serikali iokoe pesa za watanzania wanaoteseka kwa kukosa huduma mbali mbali. Asanteni.
 
Najiuliza siku zote kwani Baba wa Taifa alipoweka utaratibu wa mwenge kuzunguka nchi nzima hakueleza kinagubaga lengo/ maudhui hasa ni nini? Kunahaja ya viongozi waliopo sasa wakaueleza umma amabao wengi wao kwa sasa ni wale wa kizazi kipya, hawajui kabisa maudhui kamili ya uwepo wa huo mwenge. Nimefuatilia kwa makini sana jambo hili kwa lengo la kujiridhisha uwepo wa mwenge wenyewe bila kuhoji maudhui yake, nikagundua sio sisi tu hata ulimwengu mzima kupitia michezo ya Olympic inao mwenge tena unandege yake kabisa na ulinzi mkubwa tu. Leo hii, baada ya kuwasili Brazil jana, ambako mashindano haya yatarajiwa kufanyika, utazungushwa nchi nzima. Baada ya hapo utawekwa uwanjani kipindi chote cha mashindano huku ukiwaka na kisha utarudishwa makao makuu kungojea kipindi kingine cha mashindano. Hata sisi tunashiriki mashindano hayo hivyo tunauabudu mwenge huo lakini tunahoji uwepo wa mwenge wa kwetu. Kama nilivyosema mwanzo kunahaja ya viongozi wetu au wana JF wakafafanua nini hasa ya maudhui ya mwenge huu na kama je maudhui hayo bado yanafaa kwa sasa tukizingatia swala Zima la kujitegemea na kubana matumizi ili kujiletea maendeleo yetu. Nawasilisha tafadhali.
 
Back
Top Bottom