Kuwe na sheria itakayowabana Viongozi kutoa matamko yatakayoiingizia serikali hasara.

MGANGA MCHAWI

Senior Member
Oct 15, 2015
199
393
Imekua ni kawaida kwa viongozi wetu hasa wa vyeo vya kisiasa kutoa matamko mengi yasiofata taratibu au kutozingatia sheria ambayo mwishoni yamekua yakiingizia serikali gharama ambazo kama tu angefata taratibu isingetokea.
Tanzania ni nchi mojawapo ambayo viongozi wa kisiasa wamepewa mamlaka makubwa sana ya kuamua jambo bila hata ya kushirikisha wataalamu waliokua nao katika sekta zao.
Swala hili limejidhihirisha mara nying sana mfano PM alipokua anashughulikia swala la faru john ilionesha waz kabisa hakuusikilza kwanza wataalamu wa sekta husika kabla hajatoa tamko.Alipoagiza kaburi la faru john lifukuliwe lichunguzwe ilionesha dhahiri kuwa hana taarifa sahihi hasa pale wazr wake Maghembe alipofafanua kuwa wanyama wanaokufa bila kua na magonjwa huwa hawazkwi.
Pili swala la mh Rais kuvunja bodi ya TRA kwa kosa la kuweka fedha kwenye fixed account katika benk za biashara kwa kuwatuhumu kuwa walitaka wapige ela jambo lililokanushwa hadharani na Gavana wa benk wa kuu Prof Ndulu.
Mifano hiyo michache
Kuna waziri alishawahi kulifungia gazeti la mwanahalisi(kabla ya saiv) na wamiliki walipoenda kidai haki mahakamani wakashinda na serikali ikaamuliwa ilipe fidia a hasara waliyopata mwanahalisi ya kutochapisha gazeti kwa muda wote walipofyngiwa kwa kigezo cha waziri kutofata taratibu.
Kuna matamko mengine yanaliingizia hasara taifa sio moja kwa moja mfano waziri anapotoa tamko la kuunganisha masomo na kuingza serikali gharama ya kuandaa mitaala mipya ya elimu then baadae inaonekana agizo halitekelezeki.
Kuna kesi nyingi sana zilizosababishwa na viongozi wa kisiasa ambazo mwishoni zimeingiza hasara seriali kwa watuhumiwa kushinda kesi na kudai fidia ya kichafuliwa jina kwa kigezo tu cha kutofata taratibu.Hii inaonesha viongoz hawaombi ushauri kwa wataalamu waliokua nao kabla ya kuchukua uamuzi.Kiongozi yeyote mwenyewe busara ni lazma aangalie madhara ya maamuzi yake kisheria kabla hajatoa maamuzi.
Mh Kikwete alishawahi kunukuliwa akisema watuhumiwa wengi wa kesi waliokua nao hawana ushahidi wa kutosha hivyo wakiwapeleka mahakamani watashindwa kwa kukosa ushahidi na watuhumiwa watadai fidia na kupata hasara mara ya pili.Hii ndio busara ya kiongoz inayotakiwa.
Lazima viongoz waelewe utofauti kati ya "COURT OF LAW" na COURT OF JUSTICE".Usipokuwa na ushahidi wa kutosha mahakamani utashindwa tu na tutaendelea kulalamika mahakamani hakuna haki kila siku.Vitu vya kisheria havihitaji kukurupuka.
Kabla ya kutoa matamko viongozi wetu wanapaswa kuangalia madhara ya kisheria na hawapaswi kufanya mambo ya kisiasa.Mambo ya kisiasa wafanye na wanasiasa wenzao wasihusishe na maswala ya kitaaluma.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom