TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Kuna jambo moja ambalo watu hushindwa kutofautisha
1) Kuwaza
2) Kufikiri
Kwa kuyatazama mtu anaweza dhani ni kitu kimoja lakini katika uhalisia ni vitu viwili tofauti na 95% huwaza ila 5% ndio hufikiri.
Mawazo kila binadamu anayo ila Kufikiri ni watu wachache tu ndio wamebahatika kuingia kwenye kundi hili.
Unaweza Kuwaza namna unavyoweza kumiliki chombo cha usafiri ila mwingine akafikiria mbinu za kupata hicho chombo na namna kitakavyoweza kumsaidia na akatengeneza mpango kazi.
Kwa siku binadamu anaweza kupata Mawazo zaidi ya milioni lakini kiuhalisia kwa siku mtu asifikirie kitu. Watu wengi ni wazuri sana kwenye Kuwaza ila wengi ni wabovu kwenye kufikiria na ndipo mmiliki wa kiwanda cha magari Henry Ford aliposema "kufikiria ni kitu kigumu sana ndio maana watu wachache sana hufikiria"
Wengi hujidanganya kwa elimu zao na kudhani walicho nacho kichwani ni fikra kumbe ni Mawazo, tofautisha kati ya moshi na moto...wengi huishia kwenye moshi na sio kwenye moto.
Wanaofanikiwa wengi hufikiria na sio Kuwaza. Nenda Bar kutana na walevi au vijiweni kutana na vijana utashangaa wana Mawazo mazuri sana lakini sio kwamba wana fikra nzuri sana.
Fanyia kazi hili nawe utajiona tofauti kabisa. Acha Kuwaza na anza kufikiria.
Unawaza kujenga ghorofa lakini hufikirii kujenga ghorofa.
Niwatakie jioni njema wapendwa.
Mtenga Gerald
TAECO LTD
TANZANIA
www.facebook.com/TAECO2012