KIJICHO PEVU
Member
- May 4, 2024
- 69
- 49
KUWASHAMBULIA VIONGOZI WETU WALIOPO NA WASTAAFU KWA WATU WAO WA KARIBU KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KWA JAMII NI KUWAKOSEA ADABU
Na: Alex Msama 🇹🇿
: Agosti 1, 2025
Katika jamii inayozingatia misingi ya haki, utu na utawala wa sheria, ni jambo la aibu na la hatari kuanzisha dhana potofu kwamba ukaribu wa kifamilia na viongozi waliopo au wastaafu unamnyima mtu haki ya kugombea nafasi za uongozi. *Hili si tu ni kosa la kiakili, bali ni kosa la kikatiba na kimaadili.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inasemaje;-!!?
- Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inasema wazi:-
- Hakuna kifungu chochote katika Katiba kinachosema kuwa ukaribu wa kifamilia na kiongozi unamnyima mtu haki ya kugombea. Haki ya kugombea ni ya mtu binafsi, si ya ukoo au historia ya familia.
Sifa za Kugombea Nafasi za Uongozi wa Kijamii;-
Kwa mujibu wa Kanuni ya 15 ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
mtu anayetaka kugombea nafasi za uongozi wa kijiji, kitongoji au halmashauri anatakiwa:-
Hakuna sifa inayotaja ukoo, undugu au ukaribu na viongozi kama kigezo cha kuenguliwa.
KUAMINISHA UMMA KWAMBA UONGOZI NI NJIA YA KUNUFAIKA BINAFSI NI KOSA LA KIMAADILI NA KISHERIA
Kauli zinazodhalilisha utumishi wa umma kwa kuufananisha na njia ya kuchuma mali ni hatari kwa ustawi wa taifa. Zinapotosha dhana ya utumishi kama wito wa kujitoa kwa ajili ya jamii.
TUNASHAURI KWA HESHIMA NA MANTIKI WALE WOTE WANATAMA JAMAA AMA NDUGU WA KIONGOZI ASIPATE SIFA
1. Kwa wale wanaoamini kuwa ukaribu na viongozi iwe sababu ya kuenguliwa, tunashauri waombe mabadiliko ya Katiba kwa njia rasmi. Katiba ya sasa haijazuia mtu yeyote kugombea kwa sababu ya undugu ama ukaribu.
2. Kuwashambulia viongozi kwa maneno ya kebehi, dhihaka au shutuma ambazo kikatiba hawana wako sawa ni Kosa la kimaadili—linavunja heshima yao ya jamii
Kosa la kisheria—linakiuka haki ya msingi ya kushiriki katika shughuli za umma (Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Tanzania)
3. Tuwaheshimu viongozi wetu waliopo na wastaafu, na tuwape heshima sawa kwa familia zao. Kuwatuhumu bila ushahidi ni kuwakosanisha na jamii, na ni kinyume na utamaduni wa heshima wa Mtanzania.
HITIMISHO:-
Tujenge jamii inayotambua haki za kila mtu bila ubaguzi. Tujenge utumishi wa umma kama ibada, si kama biashara. Na tuendelee kuhimiza heshima, usawa, na mshikamano wa kitaifa.
ALEX MSAMA
Na: Alex Msama 🇹🇿
: Agosti 1, 2025
Katika jamii inayozingatia misingi ya haki, utu na utawala wa sheria, ni jambo la aibu na la hatari kuanzisha dhana potofu kwamba ukaribu wa kifamilia na viongozi waliopo au wastaafu unamnyima mtu haki ya kugombea nafasi za uongozi. *Hili si tu ni kosa la kiakili, bali ni kosa la kikatiba na kimaadili.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inasemaje;-!!?
- Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inasema wazi:-
“Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa mujibu wa Katiba."- Hakuna kifungu chochote katika Katiba kinachosema kuwa ukaribu wa kifamilia na kiongozi unamnyima mtu haki ya kugombea. Haki ya kugombea ni ya mtu binafsi, si ya ukoo au historia ya familia.
Sifa za Kugombea Nafasi za Uongozi wa Kijamii;-
Kwa mujibu wa Kanuni ya 15 ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
mtu anayetaka kugombea nafasi za uongozi wa kijiji, kitongoji au halmashauri anatakiwa:-
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na umri wa miaka 21 au zaidi
- Awe na uwezo wa kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza
- Awe na shughuli halali ya kujipatia kipato
- Awe na akili timamu
- Awe mwanachama wa chama cha siasa kinachotambulika
Hakuna sifa inayotaja ukoo, undugu au ukaribu na viongozi kama kigezo cha kuenguliwa.
KUAMINISHA UMMA KWAMBA UONGOZI NI NJIA YA KUNUFAIKA BINAFSI NI KOSA LA KIMAADILI NA KISHERIA
Kauli zinazodhalilisha utumishi wa umma kwa kuufananisha na njia ya kuchuma mali ni hatari kwa ustawi wa taifa. Zinapotosha dhana ya utumishi kama wito wa kujitoa kwa ajili ya jamii.
- Utumishi wa umma ni ibada—ni kujitoa kwa ajili ya watu wote, si fursa ya kifamilia au ya kibiashara.
- Kauli ya kwamba familia moja haipaswi kuwa na viongozi zaidi ya mmoja ni ubaguzi wa kijamii unaopingana na misingi ya usawa wa binadamu.