Kuwait yataka Israel itimuliwe katika Jumuiya ya Mabunge

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Kuwait yataka Israel itimuliwe katika Jumuiya ya Mabunge
Mei 04, 2019 15:01 UTC
Spika wa Bunge la Kuwait amesisitiza juu ya kuendelezwa juhudi za kutimuliwa utawala haramu wa Israel kutoka katika Jumuiya ya Mabunge kutokana na jinai zake unazozitenda.
Marzouq al-Ghanim amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, kuna udharura kwa Bunge la Kiarabu kufungamana na suala la kupinga kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Spika wa Bunge la Kuwait amesema kuwa, udhaifu na migawanyiko ya nchi za Kiarabu imeifanya serikali ya Marekani itangaze na kuitambua rasmi Beitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala dhalimu wa Israel na kuhamishia ubalozi wake katika mji huo kutoka mjini Tel Aviv.
Aidha ameongeza kuwa, udhaifu na mifarakano iliyoko katika nchi za Kiarabu imeifanya serikali ya Marekani pia itambue rasmi umiliki wa Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria.
Amesema kuwa, Bunge la Kuwait linaendeleza juhudi zake kuhakikisha kuwa, utawala wa kibaguzi wa Israel unatimuliwa katika Jumuiya ya Mabunge.
Spika wa Bunge la Kuwait amesisitiza pia kwamba, vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kuanza kwa kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, harakati za kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu zimeongezeka zaidi baada ya Benjamin Netanyahu kufanya safari nchini Oman Oktoba mwaka jana, hatua ambayo ilipelekea Oman iandamwe na ukosoaji mkubwa.
Tags
UTAWALA WA KIZAYUNI KUWAIT
4bshe7a3c2d8821ewzd_800C450.jpg
4bsf0550dbaf1a1e369_800C450.jpg
 
Kuna Waarabu wengi sana wanajua na wanajuta kutokuwa na uhusiano na Israel .

Issue za Palestine ni ya kuzungumza tu na kuwapatia au kuwamegea ardhi kiasi kutoka kwa nchi zao kesi iishe na Amani iwepo.. sasa wao kimya na kutwa kutoa lawama
 
Palestina si waliishapewa Gaza na West Bank, bado tena wanataka nini.? Waarabu wanahangaika nao bure, after all, wao kwanza sio waarabu.
 
Kuwait yataka Israel itimuliwe katika Jumuiya ya Mabunge
Mei 04, 2019 15:01 UTC
Spika wa Bunge la Kuwait amesisitiza juu ya kuendelezwa juhudi za kutimuliwa utawala haramu wa Israel kutoka katika Jumuiya ya Mabunge kutokana na jinai zake unazozitenda.
Marzouq al-Ghanim amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, kuna udharura kwa Bunge la Kiarabu kufungamana na suala la kupinga kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Spika wa Bunge la Kuwait amesema kuwa, udhaifu na migawanyiko ya nchi za Kiarabu imeifanya serikali ya Marekani itangaze na kuitambua rasmi Beitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala dhalimu wa Israel na kuhamishia ubalozi wake katika mji huo kutoka mjini Tel Aviv.
Aidha ameongeza kuwa, udhaifu na mifarakano iliyoko katika nchi za Kiarabu imeifanya serikali ya Marekani pia itambue rasmi umiliki wa Israel kwa miinuko ya Golan ya Syria.
Amesema kuwa, Bunge la Kuwait linaendeleza juhudi zake kuhakikisha kuwa, utawala wa kibaguzi wa Israel unatimuliwa katika Jumuiya ya Mabunge.
Spika wa Bunge la Kuwait amesisitiza pia kwamba, vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kuanza kwa kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, harakati za kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na nchi za Kiarabu zimeongezeka zaidi baada ya Benjamin Netanyahu kufanya safari nchini Oman Oktoba mwaka jana, hatua ambayo ilipelekea Oman iandamwe na ukosoaji mkubwa.
Tags
UTAWALA WA KIZAYUNI KUWAITView attachment 1088309View attachment 1088310
Saudia Nayo yasemaje????
Hahahahaha utaumia saaana na Bado.
 
Back
Top Bottom