Kuwahurumia wanyama

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
KUWAHURUMIA WANYAMA


Muislamu wa kweli ni mtu mwenye huruma. Huruma ni miongoni mwa tabia za muislamu. Chimbuko la huruma ni usafi na utakasifu wa nafsi na roho, hivyo ndiyo kusema kuwa na huruma ni nembo na alama ya kuonyesha usafi wa nafsi ya mja na utakasifu wa roho yake. Huruma ya kweli inatokana na ulaini wa moyo ambao humpelekea mja kumsamehe aliyemkosea na kumfanyia wema aliyemtendea uovu. Huruma ikijizatiti na kuthibiti moyoni ndipo hujitokeza nje athari yake. Hapo ndipo utamuona mtu aliyepambika na tabia hii ya huruma anaitumia mali yake kumsaidia mwenye shida, hutumia cheo/hadhi yake kumnusuru/kumsaidia mdhulumiwa, humsamehe aliyemkosea, humpa chakula mwenye njaa na humsaidia mgonjwa. Zote hizi ni baadhi tu ya athari za tabia ya huruma.​
Huruma ni miongoni mwa sifa za watu wa peponi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia katika Qur-ani tukufu "KISHA AWE MIONGONI MWA WALIOAMINI NA WAKAUSIANA KUSUBIRI NA WAKAUSIANA KUHURUMIANA. HAO NDIO WATU WA UPANDE WA KHERI (peponi)" [90:17-18] kuwahurumia watu ni sababu ya kupata huruma ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kauli ya Mtume Muhammad saw isemayo: "Hakika si vinginevyo Mwenyezi Mungu huwaonea huruma waja wake wenye huruma" – (Al-Bukhaariy).

Hapana shaka mtu mwenye sifa na tabia hii ya huruma hupendwa na jamii. Tabia hii ya kuoneana huruma pia ndio siri kubwa ya ushindi na mafanikio ya waislamu wa mwanzo, kwani kuhurumiana kwao ndiko kulikowapelekea kupendana mapenzi ya kweli, na mapenzi haya yakawapeleka katika mshikamano wa dhati ambao ukawafanya kuwa wamoja na nguvu. Tunasoma ndani ya Qur-ani: "MUHAMMAD NI MTUME WA MUNGU NA WALIYO PAMOJA NAYE NI WENYE NYOYO THABITI MBELE YA MAKAFIRI NA WENYE KUHURUMIANA WAO KWA WAO" (48:29)

iv/ KUWAHURUMIA WANYAMA

Wanyama ni miongoni mwa viumbe hai ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake ametuambia tuwahurumie ili watusaidie na kututumikia katika maisha yetu hapa duniani. Kwa hivyo ni wajibu wetu kuwanea huruma. Mwenyezi Mungu atuambia katika Quran tukufu: "NA (pia) AMEWAUMBA WANYAMA KATIKA HAO MNAPATA (vifaa vitiavyo) JOTO NA MANUFAA (mengine); NA WENGINE MNAWALA: NA MNAONA RAHA MNAPOWARUDISHA JIONI NA MNAPOWAPELEKA MALISHONI ASUBUHI. NA (wanyama hao pia) HUBEBA MIZIGO YENU KUPELEKA KATIKA MIJI MSIYOWEZA KUFIKA ISIPOKUWA KWA MASHAKA NA TAABU. HAKIKA MOLA WENU NI MPOLE SANA (na) MWENYE REHEMA NYINGI NA (amewaumba) FARASI NA NYUMBU NA PUNDA ILI MUWAPANDIE NA (wawe) MAPAMBO…" (16:5-8)

Utafahamikiwa kutokana na aya hizi kwamba wanyama manufaa mengi sana kwa wanadamu. Wanyama wana sifa nyingi za kimaumbile zinazoshabihiana na zile za binadamu. Miongoni mwa sifa hizo ni kushikwa na kiu na njaa, kuugua, kuona baridi au joto, kuhitajia mahala pa kulala, kuchoshwa na kazi ngumu na kadhalika. Kwasababu hizi imemlazimu mwanadamu kumuhurumia mnyama kwa kumpa chakula na maji ya kutosha, kumpa malazi mazuri, kumtibu anapoumwa, kutomkalifisha kufanya kazi asizoziweza na kutomuadhibisha wakati wa kumchinja.

Amesema Mtume Muhammad saw katika hadithi aliyoipokea Abu Hurayrah: "Wakati mtu mmoja alipokuwa akienda (njiani) akashikwa na kiu kikali sana. Akashuka kisimani akanywa maji kisha akatoka, kutahamaki akamuona mbwa akihema na kula mchanga kutokana na kiu. Akajisemea (nafsini mwake): kimempata huyu kiu kama kilichonipata mimi. Akakijaza maji kiatu chake, kisha akakishika kwa mdomo wake akapanda (kutoka kisimani kuja juu). (Akanywa) mbwa akakata kiu, akamshukuru Mwenyezi Mungu, akasamehewa yule mtu madhambi yake. Wakauliza (maswahaba): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi tunapata ujira kwa (kuwafanyia wema) wanyama? (Mtume) akajibu: "kuna ujira katika kila ini bichi (mnyama hai)" (Al-Bukhaariy).

Katika hadithi hii tunamuona mwanadamu huyu anachukua taabu anaingia kisimani kuchotea mbwa maji na kumnywesha. Yote haya yanatokana na huruma iliyomo moyoni mwa mtu yule, isingelikuwa huruma asingeweza kufanya aliyoyafanya. Tabia na kitendo chake hiki cha huruma kimekuwa ni sababu ya kusamehewa dhambi zake.
 
Jazzakallah kheir
hakika uislam haukuacha kitu....na QUR-AN NDIO MUONGOZO WETU
 
Hivi na waislam huwa wanawahurumia mbwa kwa kuwafuga?nauliza tu

Tukija katika mas-ala ya kufuga mbwa nyumbani kwetu Uislamu umetukataza isipokuwa tu ikiwa mmemfuga nje ya nyumba kwa ajili ya kuwinda au ulinzi wa nyumba. Ikiwa ni kwa ajili hiyo shari’ah imekubali kumfuga huko na kuhakikisha kuwa umemtekelezea haki zake zote kama kumpatia chakula, maji, kumsafisha na kumpeleka kwa daktari akiwa mgonjwa.
 
Back
Top Bottom