Konzo Ikweta
JF-Expert Member
- Oct 3, 2013
- 745
- 1,504
Siku moja Arthur Barry aliyekuwa mwizi maarufu wa Vito vya thamani (jewels) aliulizwa na mwandishi wa habari; ni nani ambaye unakumbuka uliwahi kumwibia sana kwenye maisha yako. Arthur Barry akasema jibu ni rahisi; niliyewahi kumwibia kwa kiasi kikubwa ni Arthur Barry kwa sababu nimetumia theluthi mbili ya muda wa maisha yangu gerezani kwa sababu ya wizi.
Lakini kama ningeamua kuwa mimi halisi kwa vitu nilivyopewa na Mungu nisingekuwa hapa nilipo leo. Ningekuwa nimefanya mambo makubwa sana. Ningekuwa nimesaidia maisha ya wengi kuwa bora zaidi.
Arthur Barry anatupa maana nyingine ya *wizi* kuwa sio kitendo cha kuchukua mali ya mwingine bila idhini yake tu bali hata kushindwa kutumia uwezo wako ipasavyo na muda ni aina nyingine ya wizi. Unajiibia mwenyewe na wengine pia kwa sababu kuna kutegemeana. Hivyo kuna watu ili wafike wanakotakiwa kufika ni lazima wewe uvuke hapo ulipo.
Lakini watu wengi hawaishi katika uwezo halisi walionao. Hawatumii muda ipasavyo. Mtu hujilinganisha na wenzake na akiona amepiga hatua moja zaidi ya wenzake anaridhika lakini kumbe kiuhalisia alitakiwa kuwa mara kumi zaidi. Penda kujitathimini mwenyewe, je huwezi kufanya zaidi ya hapo? Huo ndio uwezo wako halisi? Mabadiliko mengi huletwa na wale wanaishi uhalisia wao.
Kuna mtu anauwezo mkubwa wa kuimba mashairi lakini hafanyi hivyo. Kuna mtu anauwezo mkubwa wa kufundisha wengine lakini hataki na kuna mtu anauwezo mkubwa wa kugundua vitu lakini hataki kufanya. Laiti ungepata picha ya ukubwa wa mabadiliko utakayosababisha kama ukiwa halisi katika nafasi yako usingekubaliana na hivyo unavyoona ni vikwazo leo. Ungefahamu idadi ya watu ambao utainua maisha yao nakuhakikishia hutokubali mtu kukuchelewesha. Laiti ungefahamu aina ya marafiki na watu utakaowapata kama ukiamua kuuishi uhalisia wako kamwe usingekuwa na visingizio visivyo vya msingi.
Usikubali kuwa Arthur Barry wa pili. Simama kwenye nafasi yako. Kuwa halisi. Kuna kitu cha tofauti unacho ambacho hakuna mwanadamu mwingine anacho. Lakini ili kiwe na athari chanya (positive impacts) unatakiwa kufanya zaidi ya hapo (go extra mile). Usikubali kupoteza muda kwa kujiibia mwenyewe. Usikubali kupoteza furaha ya kesho yako kwa kujiibia mwenyewe.
#KUFANIKIWANIHAKIYAKO
@RommyTz