Kuwa shujaa wa maisha yako

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
151
250
Vitu viwili tu vikubwa ambavyo binadamu hawezi kupambana navyo..
Navyo ni siku ya kuzaliwa na siku ya kufa huwezi badilisha siku hizo daima yaani ni lazima uzaliwe na ni lazima ufe...

Binadamu anaweza kupambana na hali aliozaliwa nayo na kuifanya iwe tofauti mfano binadamu anaweza kupambana na umaskini akawa tajiri ..binadamu anaweza kupambana na kuwa anavyotaka yeye..

Watu wengi hujikatia tamaa na maisha bila kujua kua maisha ya mafanikio hayaji kwa urahisi kama wanavofikiria hawajui kuwa mda unaokata tamaa ndio mda uliokua unatakiwa ufanikiwe
Kutokua na akili darasani pasikufanye ukate tamaa ya kuwa tajiri kesho
Kuzaliwa maskini hohehahe pasikufanye ukate tamaa ya kuwa Rais wa kesho
Kuzaliwa mlemavu pasikufanye ukate tamaa ya kuwa msanii mkubwa wa kesho..

Cha msingi ni kutambua kuwa nafasi unayo bado bado hujachelewa kuwa unavotaka siku ya kuchelewa na kukata tamaa ni siku ya kifo chako tu...

Chukua hatua sasa unyanyue mguu wako wa kulia sogeza mbele kisha mguu wako wa kushoto utafata nyuma....

wekeza katika vitu vitatu vikubwa AKILI YA KUZALIWA, NGUVU ZAKO NA NIA......

Asubuhi njema kwenu

By Jay Speed
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom