Kuwa Rais, anafaa?

Kuwa Rais, anafaa?

ras mkweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
280
Reaction score
105
Kuwa Rais, anafaa?
150774_1175342565813493_9162572826720911472_n.jpg
 
Msaada wadau, Kiswahili kinanichanganya kidogo, Ipi ni sahihi kati ya hizi sentensi.....KUWA RAIS ANAFAA? au ANAFAA KUWA RAIS? au JE, ANAFAA KUWA RAIS? hii lugha inachanganya sana...ndrukiiiiiiiii
 
Ananafaa sana tu. bora huyu ana maamuzi magumu kuliko Prof. fake TEZI.
 
Anafaa sana tupo nyuma yake sisi vijana wa wilaya zote za Tanzania, natamka kama Makonda maana nae alisema alivokuwa kwenye bunge la katiba kuwa anawakilisha vijana wa Tz na mimi niwe nimetumwa sijatumwa nawakilisha vijana wa wilaya zote za Tanzania
 
Ccm mwaka huu ni shida wakimwacha el ukawa wanashinda wakimpa el ni sawa na upinzan
 
Hafai jamani ila kama tukikosa mwenye sifa za kutuongoza basi hatuna jinsi, mungu atuongoze atuvushe katika kipindi hiki kigumu na cha mpito tusije fanya kosa tukachagua mtu asiye sahihi. ni hayo
:frown::frown::frown::frown::frown::frown::frown::frown::frown:
 
Msaada wadau, Kiswahili kinanichanganya kidogo, Ipi ni sahihi kati ya hizi sentensi.....KUWA RAIS ANAFAA? au ANAFAA KUWA RAIS? au JE, ANAFAA KUWA RAIS? hii lugha inachanganya sana...ndrukiiiiiiiii

Vyote sawa..
 
Anafaa sana tupo nyuma yake sisi vijana wa wilaya zote za Tanzania, natamka kama Makonda maana nae alisema alivokuwa kwenye bunge la katiba kuwa anawakilisha vijana wa Tz na mimi niwe nimetumwa sijatumwa nawakilisha vijana wa wilaya zote za Tanzania

ha ha ha ha - inafurahisha sana kufikira vijana wa "Wilaya" zote Tanzania walikutanaje mpaka wakakuteua aisee...dah!
 
Ananafaa sana tu. bora huyu ana maamuzi magumu kuliko Prof. fake TEZI.

Nini tafsiri ya maamuzi magumu? Fisadi yeyote ana maamuzi magumu. Kuwaibia watu mchana kweupe kunahitaji maamuzi magumu. Hajali cha jela wala nini!
 
ha ha ha ha - inafurahisha sana kufikira vijana wa "Wilaya" zote Tanzania walikutanaje mpaka wakakuteua aisee...dah!

Mbona Paul Makonda kwenye bunge la katiba alisema kuwa anawakilisha vijana wote wa Tanzania wawe CHADEMA, CUF,CCM,TADEA,NCCR MAGEUZI wote kwa ujumla wao alisema anawawakilisha kwa hiyo hata akiongea pumba jua pale wameongea vijana wa Tanzania nzima maana alisema kuwa wamemtuma kwenye bunge la katiba.Sasa alikuwa amechaguliwa na nani huyo Makonda?
 
Back
Top Bottom