Kuwa na hasira mara kwa mara na kuwachukia watu bila sababu

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,845
2,020
Habarini wana JF,

Hivi tatizo la kuwa na hasira mara kwa mara na kuwachukia baadhi ya watu na hata ndugu wa karibu bila sababu yoyote tatizo huwa ni nini na ni kipi cha kufanya kuepukana na hii hali.Msaada jamani kwa anaejua mwenzenu hii hali inanitesa sana maana nakosana na baadhi ya ndugu wa karibu wengine wanalalama kuwa nawajibu harsh pia nawaonesha chuki ya wazi mimi pia sipendi hii hali hila inakuja automatic najikuta tu nina mtu ilhali sina ugomvi nae.

Ushauri please nifanyeje kuiepuka hii hali!
 
Inawezekana una msongo wa mawazo, au muda mwingi unautumia kukaa peke yako, pia inawezekana unapenda sana kukosoa yaani mtu hata akifanya jambo dogo sana unali notice na unakubali likukere. Hapo utakua unaona watu wanakuboa, unajitenga nao na kuwachukia.

Jaribu ku socialize, pia usijiweke/usijione upo juu saaaana kuliko watu waliokuzunguka hata kama umewazidi elimu ama kipato.
 
Kama ujitambua shida yako ni tiba pia karibisha tabia mpya kama upendo,kuto jali mambo ambayo hayana msingi na kufanya ibada.hiyo tabia itapungua.
 
Hizo ni stress chukua muda uanze kufanya meditation zitaisha, pia kama umetambua una hilo tatizo basi fanya viceversa yani panapo huzuni jipe furaha, panapo chuki onyesha upendo
 
Habarini wanajf,hivi tatizo la kuwa na hasira mara kwa mara na kuwachukia baadhi ya watu na hata ndugu wa karibu bila sababu yoyote tatizo huwa ni nini na ni kipi cha kufanya kuepukana na hii hali,msaada jaman kwa anaejua mwenzenu hii hali inanitesa sana maana nakosana na baadhi ya ndugu wa karibu wengine wanalalama kuwa nawajibu harsh pia nawaonesha chuki ya wazi mimi pia sipendi hii hali hila inakuja automatic najikuta tu nina mtu ilhali sina ugomvi nae,ushauri please nifanyeje kuiepuka hii hali!
Ishi maisha ya ndani ya Iman.
Jenga tabia ya kuridhika, kusamehe na kusahau.
Kumbuka kila jambo hupangwa na mungu, na hakuna ambalo litakalokutokea bila ya Mungu Kutaka.

Pitia hapa kwa Suluhisho zaidi

What causes temper, anger and having a 'short fuse' and how do you reduce or stop it? - Quora
 
Tuanze mwanzo kabisa
1. Wewe kwako pesa ni tatizo au zipo za kubadili mboga??
2. Unajua kutumia pesa? Yani namaanisha wewe ni mtu wa kula bata??
Ukijibu nitakushauri vizuri.
 
Tuanze mwanzo kabisa
1. Wewe kwako pesa ni tatizo au zipo za kubadili mboga??
2. Unajua kutumia pesa? Yani namaanisha wewe ni mtu wa kula bata??
Ukijibu nitakushauri vizuri.
Za kubadili mboga zipo pia mimi si mtu wa kula bata kiivo just normal tu
 
Kila jambo ukiamua utaweza ila huwa ni taratibu na ujiweke ahadi wewe mwenyewe kwa kusema sitarudi na siipendi tabia hii.kuna siku itaisha na kila kitu jaribu kuliona au kuitafsiri ktk mawazo chanya.
 
Yaan katika uzi ambao umejibiwa kistarabu ni huu hapa.

Big up Wakuu.

Nije kwenye point, do you have a boyfriend/lover friend? if yes jaribu kuwa naye karibu mpeane faraja maana imeonekana wanawake ambao wako single without lover friend (to put it more clear) wanakuwa na matatizo kama yako.

And if huna jaribu kuwa naye anaweza kuwa tiba yako na uje na mrejesho hapa.
 
Pole sana,jaribu kupata muda zaidi wa kupumzika haswa kulala. Forgive yourself for all wrongs you have done and try to forgive others, they are not perfect and you're not too. Kubali huwezi kubadili kila kitu na kila mtu katika jamii inayokuzunguka. Sahau yaliopita anza mwanzo mpya wa maisha, jana sio leo na wala jana haitakua kesho. Upendo is a complicated thing jaribu vitu rahisi kama kumsaidia yoyote kama unaweza au kujitoa pale inapohitajika mtu kujitolea.

All the best
 
Kila jambo ukiamua utaweza ila huwa ni taratibu na ujiweke ahadi wewe mwenyewe kwa kusema sitarudi na siipendi tabia hii.kuna siku itaisha na kila kitu jaribu kuliona au kuitafsiri ktk mawazo chanya.
Nashukuru kwa ushauri wako nitajitahidi kuufanyia kazi.
 
Back
Top Bottom