Kuwa na akili nyingi sio kuwa tajiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa na akili nyingi sio kuwa tajiri!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Aug 28, 2009.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilikuwa nikiamini katika jambo hili, kwamba watu wenye uwezo mkubwa kiakili huwa na mafanikio katika maisha.
  Nilikuwa nikiamini hivyo kwa sababu nilikuwa nikijua kwamba ni wale wenye uwezo mkubwa darasani ndio pekee wenye uwezo wa kufanikiwa katika maisha, lakini hivi karibuni baada ya kusoma tafiti kadhaa na kuangalia maisha ya wale niliosoma nao ambao darasani walikuwa wakituburuza kwa kupata maksi za juu na kufaulu sasa hivi maisha yao ni ya kawaida kabisa na wengine wameshindwa kabisa katika maisha wamebaki kubaingaiza tu mitaani.

  Wale ambao tulikuwa tukiwaita mbumbumbu, ambao hawakuwa na uwezo kabisa darasani na wengine walishindwa kabisa kuendelea na masomo wakiwa hata hawajafika darasa la tano, ndio ambao wamefanikiwa na kumudu kuwa na kipato cha kuridhisha na wengine wakiwa wanamiliki biashara kubwa kubwa.

  Na ndio maana kuna wakati unashangaa sana kusikia watu wakisema, ‘fulani alikuwa bomu kabisa darasani, hata la nne hakumudu kumaliza, lakini sasa ana fedha kama nini!’ Kwa nini kauli kama hizi zimebeba mshangao mkubwa? Ni kwa sababu, tumefanywa kuamini kwamba, uwezo wa kiakili, ndiyo unaoamua mtu apate fedha kiasi gani maishani mwake.

  Ninavyojua mimi ni kwamba, kuna watu kwa mamilioni ambao wana akili sana, kuanzia za darasani na zile za nje ya darasa. Lakini, ukiangalia kipato chao, kila siku ni kile cha kubangaiza. Ukweli ni kwamba, hakuna uhusiano kati ya akili nyingi na upataji wa fedha.

  Watu wenye uwezo wa kawaida kiakili wanaweza kuwa na mali sawa na wenye uwezo mkubwa. Haijalishi uwezo wako wa kiakili linapokuja suala la mafanikio ya kiuchumi. Kama una mtazamo chanya na unahitaji mafanikio kiuchumi, haihitaji uwezo mkubwa kiakili kuvipata hivyo.

  Hata hivyo imebainika kwamba watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili pia wana matatizo kiuchumi kiasi cha kushindwa kabisa kulipia bili na za vitu kama umeme, maji, simu na vingine hata vidogo zaidi.
  Matatizo kiuchumi yanaweza kuhusishwa na uwezo mdogo wa kutunza pesa. Tafiti za nyuma zilionesha kwamba, uwezo wa kiakili huathiri pato au pesa ambayo mtu hutengeneza kwa mwaka.

  Watu wenye uwezo mkubwa kiakili huwa na mafanikio ya juu kielimu, kicheo na hii hutokea mara nyingi. Hata Ruth Spinks, mwanasayansi wa neva (neuroscientist) anathibitisha jambo hilo na kusema, halina majadala. Na anasema, kwenye pato la kifedha, akili kubwa haina nafasi kubwa.

  Lakini pia mtu kuwa na kazi inayomlipa vizuri haimaanishi kuwa ni tajiri. Mtu anaweza kuwa na mshahara mzuri sana kwa sababu ya elimu na cheo chake, lakini je, umeshawahi kujiuliza kuhusu namna watu hawa wanavyodaiwa? Wanadaiwa sana, kwa sababu hata kutunza fedha, kwao ni shughuli pevu.
  Kwa mfano,, ingawa wanasayansi waliogundua roketi walikuwa wakipata mapato makubwa haikumaanisha kwamba wao ni matajiri kwani hawakuwa na akiba ya kutosha kulidhihirisha hilo.

  Utafiti mpya wa Zagorsky unaonesha kwamba watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili huwa hawana tabia ya kutunza pesa nyingi. Wengi wanaonekana kujali zaidi sifa za kiakili kuliko zile za kifedha. Ndiyo maana, ni vigumu kukuta wanataaluma wakiwa ndiyo matajiri katika jamii.
   
 2. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  du aisee hii ni kweli mzeiyah,, nalipwa machapaa kibao ila bado nadaiwa kinoma aseeee..... halafu kweli hawa majamaa mabright siku hz wamekuwa walimu bana teh teh teh teh
   
 3. P

  Preacher JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunapozungumzia UTAJIRI tuna maana gani?? Utajiri sio kuwa na fedha nyingi, mali nyingi etc. UTAJIRI ni hali ya utoshelevu - yaani AFYA, AMANI, MAHALI PA KUISHI PANAPOSTAHILI, CHAKULA CHA KILA SIKU KINACHOTOSHELEZA na hivi vyote uwe navyo kiasi cha kuweza kumsaidia n muhitaji mwingine (au mwenzako) - hapo unakuwa TAJIRI - lakini unaweza ukaona mtu ana PESA nyingi lakini hana AFYA, HANA AMANI - ina maana bado ni mhitaji kwa namna fulani.

  Issue ya kuwa na uwezo darasani (masomo) ni kweli hai-determine maisha ya mtu - Hii inakusaidia kupata cheti kizuri - baada ya hapo kuna safari nyingine mbele - kujipanga vizuri katika kupata mahitaji yako - hapa ukikosea direction kidogo - basi unaweza ukaishia kwenye uhitaji mkubwa.

  Hapa ndipo mtu anakata TAMAA - bila kutumia akili alizo nazo kujaribu opportunities nyingine - kama umeshindwa kwenye ajira, jaribu kujiajiri, jaribu biashara etc.

  Pia tunaposoma vitabu vya Dini - unaona watu wengi waliokuwa chini sana, Mungu aliweza kuwainua - mfano Mfalme Daudi, alikuwa anachunga kondoo ila aliinuliwa akawa Mfalme - Binti Esther alikuwa binti wa kawaida ila aliinuliwa akawa MALKIA - Yusufu alikuwa gerezeni akainuliwa akawa WAZIRI MKUU -

  Hivyo bila hata kuwa na akili za darasani - Mungu anaweza kumwinua mtu akawa TAJIRI
   
Loading...