Kuwa Mwema isikufanye usitumie Akili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,413
KUWA MWEMA ISIKUFANYE USITUMIE AKILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Wema usio na akili ni uovu. Ni upumbavu.

2. Unapomfundisha mtoto wako mambo Mema yaani kuwa Mwema usiache kumfundisha kutumia Akili katika Wema Wake.

3. Elewa watu wema wasiotumia akili ndio huonewa na kutumika vibaya na waovu wenye Akili.

4. Muovu asiye na Akili hufa mapema. Muovu asiye na akili hushambulia yeyote na kumfanyia yeyote ubaya na hivyo kuwa na maadui wengi bila tija na mwishowe hujikita anaangamia mapema.

5. Muovu mwenye Akili huishi muda mrefu. Muovu mwenye akili hujificha nyuma ya watu wema waliowajinga yaani Watu wema wasiotumia Akili.

6. Muovu mwenye akili hawezi kudhuru watu Wema wasiostahili kudhuriwa ila huwatumia kujinufaisha.

7. Muovu mwenye akili huwachonganisha Watu wema wasiotumia Akili na waovu wasiotumia Akili.

8. Muovu mwenye akili hujua wakati gani wa kumrudia muumba wake. Hivyo hujua wakati sahihi wa kutubu.

9. Kwa namna hiyo. Muovu mwenye akili huwa na ukaribu wa kisiri na Watu Wema wenye Akili. Dadeki!

10. Mtu mwema asiyetumia Akili hufikiri yeye pekee ndiye anastahili kuwa Mwema. Anafikiri ukishakuwa mbaya wewe hutakiwi kusamehewa. Huyo ni mwema asiye na akili.

11. Ni kama Nabii Yona. Yeye alikuwa mtu mwema lakini asiyetumia Akili.
Au kisa cha Mwanampotevu.
Yule mwana mwema aliyebaki nyumbani alikuwa Mwema asiye na akili.
Huku mwanampotevu akiwa mwana muovu mwenye akili.
Kwamba alipogundua amekosea, amepuyanga, amemkosea Baba yake na Mungu. Badala ya kukata tamaa yeye akaamua arudi kuomba msamaha mbele za Baba yake mzazi na Mungu wake.

12. Wakati huo ndugu yake aliyemuacha nyumbani ambaye ni mwana mwema asiyetumia Akili, alipomuona ndugu yake karejea na Mzee kamfanyia sherehe ikamuuma.

13. Watu wema Hawahesabu ubaya kwa mtu aliyeamua kuungama, kubadilika na kuwa mwema. Lakini pia hawafanyi hivyo kichwakichwa.

14. Daudi alikuwa Mtu mwema mwenye Akili.

15. Kufanya Wema bila Akili ni kumjaribu Bwana Mungu wako. Ni Makosa.

16. Watu Wema wenye Akili hawachezagi kamari. Hawabeti.
Usijaribu wema wako kwa mtu ambaye hujampima wala kumchunguza.

Kufikia hapo Sina la ziada.

TaikonMaster
Kwa Sasa Dodoma.
 
yes,
hasa nyakati hizi,
uovu mwingi umejificha na kujisitiri vyema sana kwenye wema.

ni muhimu sana kua chonjo zaidi kila wakati
 
Asante kwa tafakari Heri ya mwaka mpya mtibeli karibu mwanga bar tule bia wagogo wakarimu sana
 
Haya ndo mambo yako sasa..achana na thread za kichawachawa unapoteza focus. Hii thread ninamuona makonda kbs aisee mtu muovu kbs anayewatumia watu vibaya huwatumia watu wema kujnufaisha na kujsafisha yakiwemo maccm yote makina mwigulu aliwahi mwagia mtu tindikali ksha akawasngzia chadema..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…