Kuwa makini na biashara za mitandaoni mf. Kupatana

Kuwa makini na biashara za mitandaoni mf. Kupatana

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,315
Reaction score
8,754
Jana nilijaribu kufanya biashara na mtu kupitia kupatana akaniletea mzigo samsung j7 prime full boxed, sasa bei ilikuwa 300k nikawa na shaka, na kweli simu mpya!

Nikamwambia mshikaji naomba niikague simu vizuri akakaza kwamba ile layer ya kwenye screen isitolewe maana itaondoa upya wake. Nikataka kumwelewa ila roho ikasita tena.

Nikamwambia kama we unajiamini kwamba simu yako ni original tutoe kishingo upande akakubali, ee bwana wee kukagua simu bhana si ikawa ni copy yaani ile copy mbaya, halafu fake kabisa.

Nikamwambia mchizi bhana simu yako ni fake akaanza kujionea aibu pale hata nauli sikumpa.Japo najua ataenda kumliza boya wake huko mbele.

TUWE MAKINI UTAUZIWA BIDHAA FEKI.
 
Jana nilijaribu kufanya Biashara na Mtu kupitia Kupatana akaniletea Mzigo Samsung J7 Prime Full Boxed, sasa bei ilikuwa 300K nikawa na shaka, na kweli simu mpyaa!

Nikamwambia Mshikaji Naomba Niikague simu vizuri akakaza kwamba ile layer ya kwenye screen isitolewe maana itaondoa upya wake..nikataka kumwelewa ila roho ikasita tena.

nikamwambia kama we unajiamini kwamba simu yako ni Original tutoee kishingo upande akakubali, Eee bwana wee kukagua simu bhana si ikawa ni copy yaani ile copy mbaaaaaayaaaaaaaaaaaaaa, Halafu Faaaakeeeee Kabisaaaa!

Nikamwambia Mchizi Bhana simu yako ni Fake akaanza kujionea aibu pale hata Nauli sikumpa...Japo Najua ataenda Kumliza Boya wake Huko Mbele!

TUWE MAKINI UTAUZIWA BIDHAA FEKI.
Ulijuaje fake mzee baada ya kubandua, toa full elimu kusaidia
 
Ulijuaje fake mzee baada ya kubandua, toa full elimu kusaidia
kwanza uzoefu wa kujua tu simu maana display ilikuwa tofauti kinoma, halafu kwa kawaida storage ukiambiwa ni 32 inatakiwa iwe iidogo ya 32 au exactlly sasa fake storage inakuwa above normal ile ilikuwa 33
kingine Fake hairespond kwenye baadhi ya code za original
 
Back
Top Bottom