G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Kikao cha CC ya CCM kilichoketi jana mjini Dodoma na kuishia kuvunjika ni matokeo ya awali kabisa ya sera ambazo si sahihi anazosimamia rais Magufuli. Kwa hatua za mwanzo kabisa CCM imesambaratika huku kukiwa na msukumo wa waziwazi kumtaka Kikwete aendelee na uenyekiti hadi October mwakani ambapo ndiyo hasa muda wake kikatiba utakapofikia tamati. Kwa mara ya kwanza wana CCM hawavutiwi na mwenyekiti mpya wanayepatiwa. Hili siyo jambo jema hata kidogo.
Tuje kwenye hoja ya msingi ya kuvuja kwa kikao chenyewe.
Rais Magufuli amekuwa akiwatisha mawaziri wake kuwa wasithubutu kumsema vibaya huko maofisini kwani kuna watu maalum wametumwa kuwarekodi. Tukio la kurekodiwa mke wa waziri mmoja na kusambazwa huku rais Magufuli akipigilia msumari kwa kutoa hadharani tukio lile. Kimsingi kunaweza hata kuasisiwa kuvujishwa kwa siri za baraza la mawaziri! Hizo zote ni dalili mbaya za utawala unaotakiwa kusimamia! Ufalme mmoja haufitiniki. Kimsingi yeye ndiye kinara wa kuvujisha hata zile siri ambazo kuzitoa hadharani kunafifisha waziwazi utendaji kwa wasaidizi.
Sasa kunaweza kutokea jino kwa jino kati ya Magufuli na magwiji wa CCM ambao tuliamini kuwa wameisha ndani ya chama! Laa hasha! Ndo kwanza wameibuka na nguvu kubwa tena ya ajabu kuwahi kushuhudiwa kabla! Hawana kabisa imani na mwenyekiti mtarajiwa labda kwa sababu ya aina na falsafa ya uongozi wake. Sioni hata robo ya wana CCM wanaomuunga mkono Magufuli kupewa uenyekiti (Hata huyo Ole Sendeka ukimuangalia kwa umakini mkubwa hapendezwi kabisa na falsafa ya Magufuli kiuongozi. Wapo wanaotazama mbali ule mtindo wa Magufuli kugomba au kugombeza ikiwa ataitisha chama na kuanza kugomba au kugombeza watu. Pale atakapokuwa akitoa amri kwenye kikao kama zile anazotoa kwa wasaidizi wake.
Kimsingi Magufuli ndani ya CCM ndiko ambako hatakuwa na meno kabisa! Atapingwa waziwazi na kule wakiwa against wewe basi hata kama ni rais ujue utaishia vibaya! Hilo kwa Magufuli limeanza kuonekana waziwazi. Kimsingi haungwi kabisa mkono ndani ya CCM.