kuvimbiwa kwa mjamzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuvimbiwa kwa mjamzito

Discussion in 'JF Doctor' started by mareche, Jun 10, 2012.

  1. m

    mareche JF-Expert Member

    #1
    Jun 10, 2012
    Joined: Mar 18, 2011
    Messages: 475
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 33
    wakuu kuna madhara gani endapo mjamzito atakuwa amevimbiwa au tumbo kujaa gass naombeni msaada
     
  2. li sheng

    li sheng Member

    #2
    Jun 10, 2012
    Joined: Sep 11, 2008
    Messages: 47
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 0
    Salam,
    Tumbo kujaa gesi au kuvimbiwa ni dalili ya michubuko au vidonda vya tumbo, au tumbo kutokusaga vizuri chakula (mal-absorption) havina athari za moja kwa moja kwa mtoto lakini humuathiri mjamzito mwenyewe kwa kuwa atapata maumivu, kichefuchefu, kutapika, nakushindwa kula au kulala vizuri lakini pia endapo hatopata tiba kuna hatari ya kuongezeka kasi ya vidonda vya tumbo/ chakula kutonyonywa vizuri na kuzorotesha afya ya mama mjamzito ambayo hapo humuathiri na mtoto kwa kukosa lishe ya kutosha ambayo hutegemea kutoka kwa mama.
    Ni vizuri kumuona daktari wa mambo ya kike obstetric/gynecologist kwa kumchunguza zaidi kabla matatizo hayaja ongezeka.
    Sijui kama mchango wangu utakuwa umekuridhisha, kama ndivyo ndio lengo langu kama bado jamvi liko liko wazi kwa ufafanuzi zaidi.
    Karibu
     
  3. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #3
    Aug 22, 2012
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 32,252
    Likes Received: 15,073
    Trophy Points: 280
    mke wangu halali, gesi inamsumbua. Kenda hospitali, huko kaandikiwa magnisium. Amekula lakini hazimsaidii, je afanyaje?
     
Loading...