Kuuawa askari 8: Mh. Rais ulikuwa na wajibu mwingine zaidi ya salaam za rambirambi

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
22,133
39,079
Mh. Rais pole kwa majukumu ya kila siku kiongozi wangu. Niwe wazi kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania wengi walioshtushwa na kusikitishwa na mauaji ya kikatili ya askari pili wanane huko Kibiti. Hawa ni walinzi wetu mbali ya madhaifu waliyonayo baadhi yao lakini bado nadiriki kusema utendaji wao ndio kwa kiwango kikubwa unatufanya tulale hadi asubuhi. Naamini wakitangaza mgomo wa masaa 3 na kusiwepo mbadala wao majambazi yataigeuza nchi hii shamba la bibi kwa muda mfupi, na hata ukiweka mbadala bado tutaona kasoro nyingi kama tulizoona wakati wa mgogoro wa bomba la gesi huko Mtwara tulipoamua kushirikisha Jeshi la Wananchi kuzima maandamano ya wananchi. Kilichotokea huko wenyeji wa Mtwara ni mashahidi.
Baada ya utangulizi huo niseme ulichokifanya juzi kupitia msemaji wako maalum kutuma salaam za rambirambi kwa Waziri na IGP ni kitu sahihi na kinachotia moyo. Lakini Rais wangu hukupaswa kuishia hapo. Wewe ni Amiri Jeshi Mkuu na mlezi wa majeshi yote nchini. Kwa maoni yangu ulipaswa kuwepo leo pale Kurasini kuwaaga vijana hawa waliokufa wakiwa kazini. Unataka afe nani ndo uende? Afe Kamishina au IGP ndo utahudhuria? Katika nchi ambayo askari mmoja wa Polisi anahudumia takribani raia 1000 (kitakwimu 50,000,000/45000) askari nane kuuawa kwa wakati mmoja ni pigo kubwa. Achana na wanaokwambia ni tukio la kawaida utafikiri wameuawa punda 8 wa mfugaji. Hata punda nane wangekufa mara moja mfugaji asiona ni jambo la kawaida kama kiongozi mmoja wa polisi anavyotaka tuamini. Hivi wangeuawa twiga 8 kwa wakati mmoja Mkuu wa hifadhi angekwambia ni jambo la kawaida Mkuu, ungeona zinamtosha? Wakati mwingine washauri wako wanakukosanisha na watu wako na unaonekana usiyejali watu wako kwa sababu hawakuchagulii matukio yanayogusa hisia za watu. Unakumbuka kelele zilizopigwa ulipochelewa kwenda kuona wahanga wa tetemeko Kagera, na wasiokutakia mema wakakudanganya eti Waziri Mkuu anatosha. Hata leo naamini wamekwambia Mh. Mwiguru anatosha, hapana, tena nasema hapana, Mwiguru siyo Amiri Jeshi Mkuu, ni Mkuu wa wizara tu. Kushiriki na watu wako kwenye matatizo yao kunakufanya uonekane mwenzao na mmoja miongoni mwao. Na hata utakaposema wewe ni mtetezi wa wanyonge utapata watetezi wa kutosha na hutakuwa na haja ya kutumia Kurugenzi ya mawasiliano kujtetea. Hivi siku akifa kiongozi yeyote ya Majeshi yetu ukaonekana huko hawa wadogo watajisikiaje?
Hivyo namalizia kwa kukumbusha, wakati mwingine unapoona tukio lenye kubeba hisia za kitaifa, nenda baba hata kama haliko kwenye ratiba zako.
 
MODS: Tafadhali msiunganishe Uzi wangu na nyingine zinazohusu mauaji ya wapiganaji wetu maana huu una lengo tofauti.
 
Mkuu umeongea sahihi kabisa! Ikizingatia wanyama pori wamegeuka kuwa bora zaidi kuliko wananchi wanaowapigia kura.
Binafsi sifikirii kama hata kutuma rambirambi ilikuwa sahihi kwasababu ule msiba ni wa kwake yeye alipaswa kutumiwa pole na rambirambi kwa kuuliwa kwa askari wake,nilitegemea kusikia tamko zito kutoka kwa Rais,nilitegemea Yale magwanda ya jeshi aliyoyavaa siku ile monduli hivi Leo ndio angeyavaa na kungurumaa kwa kishindo kwa wahuni waliotekeleza mauji Yale.

Sasa kama Rais hana habari hiyo basi tutegemee kutokea mengine coz hata waziri mwenyewe sauti Yake haikuwa na msisitizo zaidi ya kuhutubia.

Makamu wa IGP wa Uganda alipo uawa Mseveni alitema cheche za kiuanaume ila huku kwetu police 8 sio chochote.
 
Mkuu Kalimbwane, asante kwa kuongeza nyama kwenye bandiko langu, ni kweli tunategemea Rais ataongelea wapi kuhusu upuuzi uliofanywa na wauaji ili wajue hawako salama huko waliko zaidi ya kwenye msiba husika? Leo suala la vyeti feki kaliongelea UDSM, sawa kabisa ni sehemu sahihi. Au maandishi yale ya Msigwa ndo yana uzito wa kutosha kukemea jambo hili zaidi ya kauli yake ya moja kwa moja? Yeye na wanaomshauri wanapaswa kubadilika.
 
Back
Top Bottom