Wanajamii, habarini za usiku bila shaka muwazima. Nakumbuka siku kadhaa zilizopita niliwaomba mnisaidie namna ya kutumia simu kama Modem, nawashukuruni wote mlionisaidia na kunipa maelekezo kwani nilidownload Nokia pc swit na kuinstall kwenye pc yangu na sasa natumia internet mwendo mdundo, kuna mwanajamii alishauri kuwa kutumia simu kama modem ni kuzuri ila naua simu, ushauri huu nauchukulia kwa makini pia. Kusema ukweli Jf ainanifundisha vitu vingi hata ambavyo sikutarajia kujifunza. Niliwapigia vodacom waliniambia simu yangu haiwezi kutumia internet. Ni kweli kama baadhi ya wana JF walivyosema costomer services waliowengi wanakaa mahali ambapo hata info. hawana kuhusiana na kile wanacho kitolea service. Nawshukuruni sana na Mungu awabariki sana.
Sio kweli kuwa unaua simu, tumia tu bila wasiwasi.
Sio kuuua simu ni kufupisha life span ya battery. Battery za simu uhai wake unakwenda per XXXX number of charges. Sasa ukitumia simu kama modem kwa muda mrefu means battery usage ya simu inakuwa kubwa.
Na unajua inapokuja suala la kureplace batter. Battery za spare quality yake mnaijua..........
Kama ni kutumia net kwa masaa kadhaa kila siku bora atafute modem tu. But kama ma ni dk 15 min au 1hr kila siku may be ni sawa.
Ni ushauri tu I stand to be corrected
Senksi wakuu, ila mimi nimetafuta Programu ya simu yangu nimekosa kabisa. Ni SAMSUNG c5212 Duos...
Sio kila simu inasupport kutumika hivi (Tethering) baadhi ya simu hazina uwezo huu na nyengine zinafungwa makusudi uwezo huu e.g iPhone na Windows Phone. So ni muhimu kuchunguza kwanza kama simu itasupport hii function.
Samsung wana software 3 za PC kutegemea na Simu yako
Kies
PC studio
New PC studio
What's new for Software & Manual SAMSUNG
Kujua utumie software ipi nenda Downloads SAMSUNG
Click mobile phone kisha chagua hadi upate yako, kutakuwa na sehemu ya downloads itakuambia Software ipi unaweza kutumia, uwezo wa kutumia hii software haimaanishi kuwa itaweza kufanya tethering maana hii software pia inafanya vitu kama kuhamisha picha, ringtones etc.
Pia kuna software ambazo sio official kama mimi nina Android ya Samsung ambayo haiwezi tethering kwa kutumia software ya Samsung ila kuna Apps unaweza kuinstall inaruhusu tethering.
So fanya research yako mwenyewe kabla ya kununua.
Kwa uchunguzi wangu hiyo simu haiwezi kutumika hivyo.
Same deal for Nokia,Motorola etc. sio kila simu inaweza.
mimi natumia simu kam amodem sasa ni mwaka wa 4 na simu ni hiyo hiyo sijawahi kuibadilisha na kuhusu suala la betri kwa kawaida ya kwangu lazima niicharge kila siku
lakini kuhusu suala la kufa sijui na mimi natumia kama saa 4 na kuendelea kila siku
sasa mkuu hapo nilipokoleza rangi pananichanganya kigodo, kama battery haijafa kwanini unacharge kila siku?
@ALL
Tunaposema kutumia simu kama modem au modem yenyewe (USB modem au something else), tunamaanisha kua data zote zinazokuja katika PC yako lazima zipite katika hiyo device (Modem) katika data hizo wamo virus wa PC na Mobile na wengineo, so hapo ndio tunasema simu inakufa kwa njia nyengine, ukiachana na ile ya betri. Usichukulie wewe pekeyako umetumia kwa muda gani simu haijafa, kwani hata wavuta sigara waliokuwa hawajaona madhara wapo na wanavuta toka 50 years iliopita.So tumia modem kama unaipenda simu yako, kwani modem ina ROM (Read Only Memory) yani virus hawezi kujiandika----ingawa inawezekana kuandika katika ROM ila hadi kwa maujuzi fulani ambayo virus ni vigumu kufanya.