Kutowajibika: Ugonjwa unaowatesa wengi…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443


Hili ni jambo muhimu sana katika maisha. Usimuachie mtu mwingine majukumu yako kwani kwa kufanya hivyo unampa pamoja na uhuru wako. Uhuru wako umo ndani ya majukumu yako, uhuru ni matokeo ya kuwajibika.

Kama huwezi kuwajibika au kubeba msalaba wako, pia fahamu kwamba, huwezi kuwa huru, utakuwa mtumwa wa huyo unayemuachia majukumu yako. Ukiwajibika utakuwa huru, na ukiwa huru utakuwa mwenye furaha na amani na utaridhika katika maisha yako. Usipowajibika utakuwa mtumwa, na ukiwa mtumwa utakuwa huna furaha, utakuwa mwenye hofu, huzuni, hasira za haraka haraka, na utakuwa mtu mwenye kuumwa mara kwa mara.

Anza kutimiza wajibu wako kwa kuanzia kwenye mambo madogo madogo na baadaye itakuwa rahisi kwako kutimiza wajibu wako hata katika yale makubwa. Lakini pia, huwa tunapewa ahadi mbalimbali na watu wetu wa karibu wakiwemo waume zetu na wake zetu. Inapotokea wameshindwa kututimizia ahadi hizo huwa tunaumia sana. Tunaumia kwa sababu ya matarajio tuliyokuwa nayo.

Ukweli ni kwamba hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kukutimiza matarajio yako. Ni wewe peke yako ndiye mwenye uwezo wa kutimiza matarajio yako kwa sababu yapo ndani yako. Unapokuwa na matarajio kutoka kwa mtu mwingine, ufahamu kwamba, mwenye kutimiza matarajio hayo siyo wewe, ila ni huyo mtu mwingine. Mtu huyo mwingine ana mamlaka ya kukutimizia au asikutimizie.

Lakini pia ukumbuke kwamba mtu huyo mwingine ana matarajio yake ambayo yanamsubiri ayatimize. Ni vigumu kukutimizia wewe matarajio yako wakati ya kwake yanamsubiri. Hivyo, usiumizwe na ahadi ulizoahidiwa na mtu mwingine hasa inapotokea akashindwa kukutimizia. Kwa maneno mengine ni kwamba usiwe mtegemezi wa ahadi kwani matokeo yake ni maumivu ya kihisia na kiakili na hatimaye ya kimwili.
 
Sasa kama kila mtu atimize wajibu wake, afu hapo hapo unasema nijitimizie mwenyewe, does not make sense to me. Kama ilikuwa ni wajibu wa mume afanye, haya mambo ya kila ajifanyie matarajio yake ni ku-justify uvizu na uzembe tu.

Sikubaliani nayo hata kidogo, kila mtu atimize wajibu wake, kama hawezi asiahidi na/au aseme kabisa hana analoweza.
 
asante kwa kutukumbusha mkuu Mtambuzi ni kweli kuna mda tunasahau wajibu wetu
 
Last edited by a moderator:
Ukweli ni kwamba hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kukutimiza matarajio yako

uongo hapo baba Ngina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…