Kutokana na sera,mipango na maamuzi tunayoyashuhudia,uelekeo wetu ni upi sasa?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
(A)Tunasonga mbele au tunarudi nyuma?

(B)Tumesimama, muelekeo ni kusonga mbele?

(C)Tumesimama,muelekeo ni kurudi nyuma?

(D)Hatujasimama,muelekeo ni kusonga mbele?

(E)Hatujasimama, muelekeo ni kurudi nyuma?

(F)Haileweki,tumesimama, hatujasimama,tunarudi nyuma au tunasonga mbele?

Maswali yote haya ni kutokana na kuwaza haya.

Nawaza tumbua huku tukienndelea kwalipa mishahara.

Nawaza fukuza wenye vyeti feki huku nafasi wanazoziacha hazijajazwa.

Nawaza zitajazwa lini na itachukua muda gani

Najua mishahara yao ipo lakini nawaza zilipo hela za kuwalipa fedha za kujikimu waajiriwa wote wapya.

Nawaza athari za zoezi hili

Nawaza kupungua kwa mizigo bandarini.

Nawaza kufungwa kwa biashara nyingi

Nawaza kuhusu ununuzi wa ndege

Nawaza kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa

Nawaza kuhusu sera ya viwanda

Nawaza kuhusu umeme wetu

Nawaza ukubwa wa bajeti yetu

Nawaza utekelezaji wake

Nawaza kuhusu makusanyo

Nawaza tukilazimika kuendekea kukopa

Nawaza deni la Taifa lilliopo sasa

Nawaza pa kupata mikopo

Nawaza makato ya asilima 15 kwa ajiili ya deni la Bodi ya Mikopo

Nawaza hali ya baadhi ya mabenki ya kibiashara

Nawaza watumishi kuendelea kutoongezewa mishahara.

Nawaza kuhusu utawala wa sheria

Nawaza kuhusu utawala bora

Nawaza kuhusu elimu bure na utekelezaji wake.
 
Back
Top Bottom