BigBro
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 3,478
- 11,023
Habari Wakuu, Leo Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ndiye mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA)
Utekelezaji wa miradi huu ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam. Mkandarasi Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd, ndiye anayejenga Barabara hii kwa gharama za shilingi Bilioni 87.156 na ujenzi wake utadumu kwa miezi 35.
Nitawapa Updates nipo eneo la tukio. Kwa sasa wimbo wa Taifa ndo unaimbwa.
Hivi ndivyo itakavyoonekana baada ya kujengwa