Kutoka nje ya ndoa

mtzmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
8,704
Reaction score
9,079
Wana mmu kwa nionavyo mie wote wanaotoka nje ya ndoa zao walikurupuka kuoa/kuolewa na hawajui maana ya ndoa ni nn walifunga ndo kwa sifa tu ndo mana yanatokea hayo.
 
Wana mmu kwa nionavyo mie wote wanaotoka nje ya ndoa zao walikurupuka kuoa/kuolewa na hawajui maana ya ndoa ni nn walifunga ndo kwa sifa tu ndo mana yanatokea hayo

Pamoja na kuwa umeamkia asubuhi tu na hoja hii ya mapenzi (nadhani ungelisubiri angalau watu wakapanga mawazo ya kazi za leo za kuleta mkate wa leo), si kweli kuwa wanaofanya hayo walikurupuka! Itafakari zaidi reasoning yako!
 
Napinga sana matumizi ya viroba,haiwezekani mtu aanzishe thread haina kichwa wala miguu
 
Oa kwanza huo mpango wa kando usiuongelee
tu kwa uzoefu wa kusikia tu. Ingia kwanza.

Halafu ni wake kwa waume huwa mpango ni
wa Kando kila uchao.
 
kwani jana ulikunywa chupa ngapi.....???
kijana hebu jipange kwanza so unakurupuka kurupuka!!!
 
tatizo la kulalia viroba vya ofa na godoro la ambiance unakurupukia tu jf.
 
Oa kwanza.....halafu uje na uzi wako hapa......usipopiga unapigiwa....
 
hata kama maini matamu vp lazima kuna cku utataman maharage oa kwanza ndio utaelewa kwa nn ni lazima utoke nje!!!
 
Wana mmu kwa nionavyo mie wote wanaotoka nje ya ndoa zao walikurupuka kuoa/kuolewa na hawajui maana ya ndoa ni nn walifunga ndo kwa sifa tu ndo mana yanatokea hayo

Utamwomba mkeo Kabang?
 
Hakuna anayeingia kwenye ndoa akiwa na wazo la kutoka nje. Kila anayefanya hivyo ana mwanzo wa safari hiyo. Oa uone utamu wake.
 
kwa wanaume: mwanamke mmoja hatoshi, lazima tuwe na wa nje :eyeroll1:

kwa wanawake: figa moja haliivishi chakula :eyeroll1:
 
kuna thread nyingi zimeanzishwa humu nyingi tu kwa nini wanandoa wanatoaka nje.
 
Kutoka nje ya ndoa isichukuliwe kuwa ni kukutana kimapenzi na mtu mwengine asiye mke au mume uliyefunga naye ndoa...inaenda mbali mpaka "kutoa hata siri za ndani ya ndoa nako ni kutoka nje ya ndoa"...

Na kwahili imethibitika kiana mama ndio wanao-ongoza kwa kutoka nje ya ndoa ..tafakarini kisha muchukuwe hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…