Kutoka Moyoni kuunga mkono huu utawala mimi imetosha sasa tusubiri 2020 tubadili tuone

mockers

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
12,806
35,229
Wakuu Salam,

Sitomuunga mkono huyu Rais na hii ni uhuru wangu kwa kua sio lazima aungwe mkono na watu wote, nasubiri 2020 nibadili wa kumuunga mkono atayekua na dira, ambae atakua msikivu kwa maslahi ya taifa.

Mdogo wangu hajaajiriwa hadi leo, mtoto wangu hana mkopo wakati anavigezo, mke wangu analia makato kwenye mishahara yao, wateja hakuna na bidhaa karibu zote zimepanda bei hadi mara 3.
 
Hakuna kitu cha hovyo maishani Kama mtu mzima mwenye familia kuwa mdaku na mzandiki.
 
Kwa hiyo umekubali Rais anao uwezo wa kuleta mabadiliko na si mfumo?
Tatizo kelele za kuimba mabadiliko ndizo zilizofanya rais afanye mabadiliko bila kuangalia mabadiliko hayo yanaelekea wapi na sasa tumejikuta tupo upande wa maumivu, sasa tupazeni tena sauti kwa sana ili astuke, tugeukie upande wa neema!
Kuhusu kutokumchagua 2020 hakuwezi kumuondoa ikulu, labda tubadili katiba na mbaya zaidi katiba sio kipaumbele chake!
 
Wakuu Salam.
Sitomuunga mkono huyu Raisi na hii ni uhuru wangu kwa kua sio lazima aungwe mkono na watu wote, nasubiri 2020 nibadili wa kumuunga mkono atayekua na dira, ambae atakua msikivu kwa maslahi ya taifa,
Mdogo wangu hajaajiriwa hadi leo, mtoto wangu hana mkopo wakati anavigezo, mke wangu analia makato kwenye mishahara yao, wateja hakuna na bidhaa karibu zote zimepanda bei hadi mara 3.
Sisi wachambuzi wa migogoro hichi ulichokiandika hapa kinaitwa "issues" alafu unataka kutumia uchaguzi mkuu kama "source " ukiamini mke wako hatokakatwa makato, mtoto wako pia ataajiliwa na n.k! Subira yavuta kheri mkuu, tuipe muda serikali.
 
Upo sawa mkuuu
 
Imetosha imetosha habari za kukimbizana na akina wema , masogange na wanaotukana kwenye dala dala na kuzifanya kua ajenda za kitaifa hapana tushtuke

Hili lakukimbizana na kina Wema mara Masogange aka wauzi k maarufu halafu ndio agenda kuu kwa taifa kama hili masikini kiukweli tumechemsha..

Kiukweli tuna vitu vingi sana kama taifa tunahitaji kuvifanya agenda na si huu upuuzi.. Binafsi pia kura yangu siwezi kumpigia huyu jamaa tena 2020 kwa mwendo huu, ni bora nimchague Hashim Rungwe.
 
Nasubiri 1 may. Nione wafanyakazi watasusa au watashangilia. Time will tel
 
Mtu mwema aliye na matatizo ya akili,anaweza kuvaa hata nguo bila kuzifua,na akala mlo mmoja tu,akikunyima wewe sabuni,na milo mitatu sioni kama anastahili kuhukumiwa bali amekupimia kipimo kile kile anachojipimia
 
Wakuu Salam,

Sitomuunga mkono huyu Rais na hii ni uhuru wangu kwa kua sio lazima aungwe mkono na watu wote, nasubiri 2020 nibadili wa kumuunga mkono atayekua na dira, ambae atakua msikivu kwa maslahi ya taifa.

Mdogo wangu hajaajiriwa hadi leo, mtoto wangu hana mkopo wakati anavigezo, mke wangu analia makato kwenye mishahara yao, wateja hakuna na bidhaa karibu zote zimepanda bei hadi mara 3.

Sawa ila sie tutamuunga mkono kwani anafanya yale tuliyotaka watanzania atufanyie. Rais Magufuli ni chaguo la Mungu kwetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom