Kutoka Mezani kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
622
1,543
MAPATO YA NDANI YA SERIKALI ZA MITAA MASHAKA MATUPU.

Nipo kwenye ziara ya kutembelea kata za Jimbo la Kigoma Mjini katika utaratibu niliojiwekea wa kushauriana na wananchi kila mwaka kabla ya Bunge la Bajeti.

Jambo moja kubwa ambalo nimekutana nalo ni malalamiko ya Wananchi kuhusu huduma za manispaa yetu ikiwemo kuchelewa kwa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara za mitaa ( Kigoma ina mvua nyingi Sana kiasili kwa hiyo Mitaa huharibika mno na makorongo kujengeka katikati ya baadhi ya mitaa ).

Nimewaambia wananchi kwamba uwezo wa Mapato wa Manispaa yetu ni mdogo mno. Tulikuwa na Matarajio ya kukusanya tshs 3.4 bilioni mwaka 2016/17 baada ya kufanya mabadiliko ya tozo na ushuru mbalimbali.

Hata kabla ya mwaka wa fedha kuanza Halmashauri zote nchini zikanyanganywa chanzo cha Mapato cha Kodi za Majengo ( Property Taxes ).

Kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji hili ni punguzo la shilingi 1.2 bilioni kutoka katika makadirio yake. Baadaye Serikali ilitangaza kwamba mapato haya yatarejeshwa kwenye Manispaa zetu, lakini mpaka sasa hakuna thumni iliyorejeshwa.

Nimewaambia wananchi kwamba hata Hizo zilizobakia shilingi 2.2 bilioni nazo tumeshindwa kuzikusanya kwa sababu Waziri wa TAMISEMI ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano hajaidhinisha sheria ndogo tulizowasilisha kwake.

Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa na Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ( sheria namba 7 na 8 za 1982 ) ni lazima Waziri wa TAMISEMI aidhinishe sheria ndogo ndipo zianze kutumika.

Manispaa yetu na Manispaa nyengine nchini zimeshindwa kukusanya vyanzo vipya vya mapato na tozo mpya kwa sababu Rais hajasaini Sheria ndogo na hivyo kukosesha Mapato Halmashauri zetu.

Sisi Kigoma Ujiji Manispaa tumeshapoteza theluthi nyengine ya Mapato ( shilingi 1bn ) kwa uchelewaji huu peke yake.

Kwa Mapato ya ndani ya Manispaa zetu nchini, mwaka 2016/17 ni mwaka uliopotea ( A Year Lost ) katika kipindi cha uongozi wa nchi unaopigania Sana mapato kuongezeka.

Hata Fedha za maendeleo kutoka Serikali kuu kuja kwenye Manispaa zimekuwa ni kidogo Sana. Kwa mfano Kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji mwaka 2016/17 tulitarajia kupata shilingi 9.9 bilioni Kama ruzuku ya miradi ya Maendeleo lakini hadi Desemba 2016, tulikuwa tumepata shilingi 1.4 bilioni tu sawa na 14.14% ya Bajeti.

Katika mazingira Kama haya Manispaa haiwezi kuleta Maendeleo Kwa watu wake isipokuwa Kwa miradi ya wafadhili tu. Baadhi ya Wafadhili wanaosaidia na watakaosaidia Kigoma Ujiji ni pamoja na Benki ya Dunia na Serikali ya Ubelgiji ( miundombinu na Hifadhi ya Jamii), Serikali ya Kuwait ( Kilimo), Serikali ya Uingereza ( Elimu- EQUIP na P4R ), Serikali ya Danmark ( Mazingira ya Uwekezaji ) na Shirika la PSPF ( Uwekezaji wa The Great Lakes Gateway Market - Mwanga Sokoni).

Manispaa nayo inajitahidi kuongeza vyanzo vya mapato na kuanzisha miradi ya kukuza uzalishaji ikiwemo Mfumo wa Hifadhi ya Jamii ili kuwezesha wananchi kuweka akiba, kupata bima ya afya na kupata mikopo nafuu.

Kujenga Manispaa ya Kijamaa katika dimbwi la Sera za kibepari ni changamoto kubwa tunayokumbana nayo kama ACT Wazalendo Hivi sasa.

Miradi mingine ni Kilimo cha Michikichi kuzalisha Mawese na Ujenzi wa Ujiji City. Hata hivyo bado tunahitaji vyanzo vya Sasa vya Mapato ili kukuza vyanzo Hivi vipya. Naomba nashauri mambo mawili;

Ninamsihi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, airudishe TAMISEMI eneo lake la asili ambalo ni Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwezesha ufanisi wa kutoa huduma Kwa wananchi. Mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Bajeti unaonyesha kwamba Rais ana mambo mengi Sana na majukumu makubwa mno.
Vinginevyo tunakwenda kupoteza mwaka mwengine.

Waziri Mkuu atakuwa na nafasi zaidi ya kusaini Sheria ndogo za Mamlaka za Serikali za Mitaa na pia kuweza kufuatilia utekelezaji wake Kwa umakini na ukaribu mkubwa.

Natumai kwamba Bajeti ya mwaka 2017/16 itarejesha kodi za majengo ( property taxes ) Kwa Manispaa na Majiji yetu nchini.

Hii itawezesha Halmashauri zetu kukusanya mapato ya kutosha kuweza kutoa huduma kwa wananchi wetu.

Tuchukulie kuwa mwaka 2016/17 ulikuwa mwaka wa majaribio na 2017/18 tuanze kazi. Bila uimara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, nchi haitakwenda. Tusijidanganye Kabisa.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma Mjini
 
Tuchukulie kuwa mwaka 2016 - 2017 ulikuwa wa majaribio.......ha ha ha ha hii nimeipenda.......bila shaka ulikuwa mwaka wa majaribio kwenye kila kitu.
 
Watanzania wote tungekuwa tunafanya maamuzi kulingana na facts observed......CCM isingalikuwapo madarakani.
 
Pole sana Zitto na wakazi wa manispaa ya kigoma- ujiji, lakini tatizo hilo ni kwa nchi nzima yaani ukiangalia miradi mipya ya maendeleo kwa mwaka2016/17 ni michache sana hivyo kuwa mbunifu,tafuta wafadhili na ibane serikali ilete ruzuku .Japo kwa DSM twajua hata wafadhili waliotafutwa kusaidia maendeleo serikali iliwazuiakwa itikadi za vyama.Kimsingi TZ bado tuna sagari ndefu kufikia mafanikio ya kweli
 
Mimi sijalibiwi!;
Tunafanya majaribio kwa miaka mitano ya kwanza kwa kutumbua majipu, na miaka mitano ya awamu ya pili ndipo tutakapotekeleza miradi
wambie wananchi wafanye kazi waache kulalamika!
kama hawataki, shika peleka kwenye makambi, wakafanye kazi kwa nguvu!
 
Lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhujumu halmashauri na majimbo yote yanayoongozwa na upinzani kwa matumaini ya kushinda majimbo na kuongoza halmashauri zote ifikapo 2020.
 
Jamaa mmoja kanambia kuwa, kule kwao Mzee wa kaya yuko radhi walale njaa kwa kukosa chakula ilhali zizini kuna ng'ombe buku.
Naona ni kweli jamaa anapenda kuna mihela imejazana hazina ilhali maendeleo katika h/shauri zetu ni zero, no ajira, no kupanda madaraja, no increments nk
 
MAPATO YA NDANI YA SERIKALI ZA MITAA MASHAKA MATUPU.

Nipo kwenye ziara ya kutembelea kata za Jimbo la Kigoma Mjini katika utaratibu niliojiwekea wa kushauriana na wananchi kila mwaka kabla ya Bunge la Bajeti.

Jambo moja kubwa ambalo nimekutana nalo ni malalamiko ya Wananchi kuhusu huduma za manispaa yetu ikiwemo kuchelewa kwa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara za mitaa ( Kigoma ina mvua nyingi Sana kiasili kwa hiyo Mitaa huharibika mno na makorongo kujengeka katikati ya baadhi ya mitaa ).

Nimewaambia wananchi kwamba uwezo wa Mapato wa Manispaa yetu ni mdogo mno. Tulikuwa na Matarajio ya kukusanya tshs 3.4 bilioni mwaka 2016/17 baada ya kufanya mabadiliko ya tozo na ushuru mbalimbali.

Hata kabla ya mwaka wa fedha kuanza Halmashauri zote nchini zikanyanganywa chanzo cha Mapato cha Kodi za Majengo ( Property Taxes ).

Kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji hili ni punguzo la shilingi 1.2 bilioni kutoka katika makadirio yake. Baadaye Serikali ilitangaza kwamba mapato haya yatarejeshwa kwenye Manispaa zetu, lakini mpaka sasa hakuna thumni iliyorejeshwa.

Nimewaambia wananchi kwamba hata Hizo zilizobakia shilingi 2.2 bilioni nazo tumeshindwa kuzikusanya kwa sababu Waziri wa TAMISEMI ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano hajaidhinisha sheria ndogo tulizowasilisha kwake.

Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa na Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ( sheria namba 7 na 8 za 1982 ) ni lazima Waziri wa TAMISEMI aidhinishe sheria ndogo ndipo zianze kutumika.

Manispaa yetu na Manispaa nyengine nchini zimeshindwa kukusanya vyanzo vipya vya mapato na tozo mpya kwa sababu Rais hajasaini Sheria ndogo na hivyo kukosesha Mapato Halmashauri zetu.

Sisi Kigoma Ujiji Manispaa tumeshapoteza theluthi nyengine ya Mapato ( shilingi 1bn ) kwa uchelewaji huu peke yake.

Kwa Mapato ya ndani ya Manispaa zetu nchini, mwaka 2016/17 ni mwaka uliopotea ( A Year Lost ) katika kipindi cha uongozi wa nchi unaopigania Sana mapato kuongezeka.

Hata Fedha za maendeleo kutoka Serikali kuu kuja kwenye Manispaa zimekuwa ni kidogo Sana. Kwa mfano Kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji mwaka 2016/17 tulitarajia kupata shilingi 9.9 bilioni Kama ruzuku ya miradi ya Maendeleo lakini hadi Desemba 2016, tulikuwa tumepata shilingi 1.4 bilioni tu sawa na 14.14% ya Bajeti.

Katika mazingira Kama haya Manispaa haiwezi kuleta Maendeleo Kwa watu wake isipokuwa Kwa miradi ya wafadhili tu. Baadhi ya Wafadhili wanaosaidia na watakaosaidia Kigoma Ujiji ni pamoja na Benki ya Dunia na Serikali ya Ubelgiji ( miundombinu na Hifadhi ya Jamii), Serikali ya Kuwait ( Kilimo), Serikali ya Uingereza ( Elimu- EQUIP na P4R ), Serikali ya Danmark ( Mazingira ya Uwekezaji ) na Shirika la PSPF ( Uwekezaji wa The Great Lakes Gateway Market - Mwanga Sokoni).

Manispaa nayo inajitahidi kuongeza vyanzo vya mapato na kuanzisha miradi ya kukuza uzalishaji ikiwemo Mfumo wa Hifadhi ya Jamii ili kuwezesha wananchi kuweka akiba, kupata bima ya afya na kupata mikopo nafuu.

Kujenga Manispaa ya Kijamaa katika dimbwi la Sera za kibepari ni changamoto kubwa tunayokumbana nayo kama ACT Wazalendo Hivi sasa.

Miradi mingine ni Kilimo cha Michikichi kuzalisha Mawese na Ujenzi wa Ujiji City. Hata hivyo bado tunahitaji vyanzo vya Sasa vya Mapato ili kukuza vyanzo Hivi vipya. Naomba nashauri mambo mawili;

Ninamsihi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, airudishe TAMISEMI eneo lake la asili ambalo ni Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwezesha ufanisi wa kutoa huduma Kwa wananchi. Mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa Bajeti unaonyesha kwamba Rais ana mambo mengi Sana na majukumu makubwa mno.
Vinginevyo tunakwenda kupoteza mwaka mwengine.

Waziri Mkuu atakuwa na nafasi zaidi ya kusaini Sheria ndogo za Mamlaka za Serikali za Mitaa na pia kuweza kufuatilia utekelezaji wake Kwa umakini na ukaribu mkubwa.

Natumai kwamba Bajeti ya mwaka 2017/16 itarejesha kodi za majengo ( property taxes ) Kwa Manispaa na Majiji yetu nchini.

Hii itawezesha Halmashauri zetu kukusanya mapato ya kutosha kuweza kutoa huduma kwa wananchi wetu.

Tuchukulie kuwa mwaka 2016/17 ulikuwa mwaka wa majaribio na 2017/18 tuanze kazi. Bila uimara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, nchi haitakwenda. Tusijidanganye Kabisa.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma Mjini
Nasubiri maoni ya Zitto kuhusu suala la Bashite.
 
Mshughulikieni aliye divert mapato ya halmashauri yaende hazina kuu kinyume na utaratibu.
 
Back
Top Bottom