Kutoka Mahakamani: Mbunge wa Arusha Godbless Lema apata dhamana

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Ni asubuhi tena kwa mbali jua limeanza kuchomoka huku Arusha ikiwa ni siku ya kupatiwa haki kwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema baada ya kuwekwa kizuizini kwa takribani miezi ninachoamini ni kwamba Mahakama kuu leo itatenda haki kwa Lema

Ulinzi nje eneo la mahakamani umeimarishwa sana.
Wananchi wamezuia kuingia mahakama kwenda kusilikiza kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema.

Waandishi wa habari wawili tukiwa nje ya eneo la mahakamani tumekamatwa na Jeshi la Polisi .tumeshikiliwa kwa muda lisaa baada ya majadiliano wahusika tumeachiwa tumezuia kuingia mahakamani.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema akishuka kwenye gari kuingia mahakamani.

Nje eneo la mahakamani wananchi zaidi 23 wamekamatwa na Jeshi la Polisi muda huu wakiwa nje la mahakamani baada ya kuzuiwa kuingia mahakamani kusilikiza kesi ya Mbunge Godbless Jonathan Lema.

Kutoka mahakamani
Wakili wa Serikali ameomba dakika 15 kuwasilisha hoja na Wakili Msomi Peter Kibatala amekubali na kuomba wapewe saa 1 kujibu so Mahakama imehairishwa mpaka saa 7 mchana

Kutoka mahakamani "Virungu vinatembea mahakamani muda huu,watu wanapigwa ,wengine wamekamatwa wamepelekwa central.
Magari ya kuwasha,police wapo na silaha nzito.

Watu wamezuiliwa kuingia,maeneo ya nje ya mahakama ni virungu".

tmp_23435-FB_IMG_14885247387692090696793.jpg

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Edward Lowasa, Waziri Mkuu Msaatafu Sumaye na Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro wakiwa mahakamani .
tmp_23435-FB_IMG_1488525644504-1345217214.jpg

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe Naibu Katibu Mkuu Chadema John Mnyika ,pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa mahakamani leo.
View attachment 476314
tmp_7995-FB_IMG_14885273469431093721955.jpg


Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa nje ya Mahakama Kuu ya Arusha baada ya Mawakili wa Jamuhuri kuomba kuwasilisha hoja ambayo wamekwenda kuiandaa kwa dakika 15 na Jopo la Mawakili wa Utetezi likiwakilishwa na Wakili Msomi Peter Kibatala,wameomba dakika 60 ili kujiandaa kujibu hoja hiyo ya mawakili wa Jamuhuri..
tmp_13412-FB_IMG_1488537019231711232815.jpg

Mahakama Kuu Arusha inatarajia kutoa maamuzi ya dhamana na Godbless Lema saa saba na nusu mchana. Mawakili wamepewa muda kujibu hoja zilizotolewa.

Viongozi mbalimbali wa Chadema wanaanza kuingia mahakamani kusubiri uamuzi wa Jaji Magimbi kuhusu dhamana ya Mbunge Godbless Jonathan Lema.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema. Ameachiwa kwa dhamana ya masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni moja.

 
Wewe ndio utafungwa miezi kumi .maana hujui sheria na hujui chochote ni kilaza dhamana ilikuwa wazi isipokuwa ni kumkomoa mtu tu ila zaidi ya yote wote walio fanya hivyo hakuna hata mmoja anaejua kesho ni mungu pekee.muda utafika maana siku hizi hachelewi kabisa.wewe furahia sheria kupindishwa ila nakwambia atafanyiwa mtu wako ndio utafurahia vema.Take care hii ni Tanzania kuna wakati hatujui tuko wapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom