Kutoka CCM Kirumba: Full time Toto Africa 0 - 0 Simba FC

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,338
Simba imeshindwa kuifunga Toto African uwanja wa CCM Kirumba kwa miaka 7 sasa, wamelazimishwa sare tasa (0-0)


KIKOSI CHA SIMBA VS TOTO AFRICAN, LEO.


1.Daniel Agyei

2.J Bukungu

3.Mohammed Shabalala

4.Juuko Murshid

5.Novart Lufunga

6.James Kotei

7.Shiza Kichuya

8.Mzamiru Yassin

9.L Mavugo

10.Frederick Blagnon

11.Mo Ibrahim


Sub


1. Peter Manyika Jr

2.Hamadi Juma

3.Jonas Mkude

4.Mwinyi Kazimoto

5.Ibrahim Ajibu

7.Juma Liuzio


Staff

1.Joseph Omog (Head Coach)

2.Jackson Mayanja (Assistant Coach)


3. Iddi Salim (Goalkeeper Coach)

4. Mussa Mgosi (Team Manager)
PhotoGrid_1492271068984.png

FULL TIME:

Dakika ya 90 + 5: Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo ni 0-0, Simba sasa inafikisha pointi 62 katika michezo 27, Toto imefikisha pointi 26 katika michezo 26.

Dakika ya 90: Zimeshaktika dakika tatu za nyongeza na mchezo hauna kasi, Toto wanacheza taratibu tofauti na Simba ambao wanacheza kwa presha.

Dakika ya 90: Mwamuzi anampa kadi ya njano beki wa Toto, Hamim kw akuchelewesha mpira maskusudi wakati wa kuurusha.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 5 za nyongeza.

Dakika ya 87: Simba wanapata faulo nje kidogo ya lango la Toto.

Dakika ya 85: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 80: Shangwe za mashabiki wa Simba zimeanza kupungua kwenye uwanja huu wa Kirumba, wale wa Toto wanaendelea kushangilia.

Dakika ya 75: Simba wanapata faulo lakini inakosa madhara kwenye lango la Toto.

Dakika ya 71: Ajibu anapiga shuti linagonga mwamba na kurejea uwanjani kisha walinzi wa Toto wanaokoa.

Dakika ya 70: Mchezo unaendelea kwa kasi, lakini upinzani na mkali zaidi.

Dakika ya 66: Mchezo unaendelea kuwa mgumu, kila timu sasa inacheza kwa umakini.

Dakika ya 58: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Laudit Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Ibrahim Ajibu.

Dakika ya 50: Mchezo ni mgumu kwa pande zote, inavyoonekana pande zote zinasomana.

Dakika ya 48: Simba ndiyo ambao wanafika langoni mwa Toto tangu kuanza kwa kipindi cha pili.

Kipindi cha pili kimeanza hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

MAPUMZIKO

Dakika ya 45: Zimeongezeka dakika 4, na mwamuzi amepuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza. Sasa ni mapumziko matokeo bado 0-0.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 43: Kichuya anampiga kanzu beki wa Toto kisha anaubetua mpira kutoka pembeni ya uwanja, unampita kipa lakini mabeki wa Toto wanawahi na kuokoa.

Dakika ya 39: Mavugo anapata nafasi ya kupiga shuti lakini linatoka nje ya lango la Toto.

Dakika ya 38: Mchezo umetawaliwa na kasi kutoka pande zote

Dakika ya 34: Simba wanafanya shambulizi kali, Blagnon anapata nafasi, anapiga shuti kali la chini, linapita pembeni ya lango la Toto.

Dakika ya 32: Lusajo wa Toto anaonyesha mbwembwe akiwa pembeni ya uwanja kwa kuwatoka mabeki wa Simba lakini baadaye wanaugusa mpira unatoka nje.

Dakika ya 30: Mchezo umeendelea, kila upande unajipanga kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza, matokeo bado ni 0-0.

Dakika ya 28: Kiungo wa Simba, Kotei anachezewa faulo katikati ya uwanja, mwamuzi anasimamisha mchezo kuwaita madaktari kumpatia tiba.

Dakika ya 25: Toto wanapata nafasi ya kupiga shuti kali linatoka hatua chache kwenye lango la Simba.

Dakika ya 22: Simba wanapata faulo nje kidogo ya lango la Toto baada ya mabeki wa Toto kumchezea vibaya Zimbwe Jr. Inapigwa faulo lakini haina madhara.

Dakika ya 20: Mavugo anamminya beki wa Toto kisha anapiga shuti kali linatoka pembeni kidogo ya lango la Toto.

Dakika ya 19: Mohamed Ibrahim wa Simba anaingia na mpira langoni mwa Toto lakini mabeki wanawahi na kuokoa.

Dakika ya 16: Toto wanafanya shambulizi kali, wanapata nafasi lakini kichwa cha straika wao kinapaa juu ya lango, matokeo bado ni 0-0.

Dakika ya 13: Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Manyanja anasimama kutoa maelekezo.

Dakika ya 10: Mchezo unaendelea huku mashabiki wakizidi kumiminika ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba hapa Mwanza.

Dakika ya 8: Toto wanafanya shambulizi langoni mwa Simba, Wazir Jr anapata nafasi ya kupiga shuti langoni mwa Simba lakini linatoka nje.

Dakika ya 5: Mchezo unaendelea kwa kasi, idadi ya mashabiki ni wengi na wanashangilia kwa nguvu. Wale wa Simba nao wapo wengi uwanjani hapa licha ya kuwa timu yao ipo ugenini

Dakika ya 1: Mchezo umeanza kwa kasi. Timu zote zinasomana.

Mchezo ndiyo umeanza

Timu zimeshaingia uwanjani ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
Wakuu mpira umekwisha kwa simba na toto kugawana pointi moja moja
 
Ft 0-0

Game ya kwanza rufaa fc 1 Kagera sugar 2
hapa walikata rufaa

Game ya pili Rufaa fc 3 mbao fc 2
hapa Mbao fc wamemsimamisha kipa kwa kosa la kuuza mchezo

Game ya tatu rufaa fc o toto 0.
hapa sijui nini kitatokea hawachelewi kukimbilia Fifa kusema Toto wamemchukua kocha wa timu nyingine.

Chezeni mpira acheni kupenda mbeleko,mbeleko ikichoka inatabia ya kutoboka.
 
Back
Top Bottom