Kutoelewana ndani ya mahusiano


Ili kuzuia matatizo ya kutoelewana, dawa kamili ni mapenzi ya kweli. Kama mlikuwa mnapendana kwa dhati, hamtachokana. Watu wanaishi maisha bwana!
 
...kuchokana kupo sana tena, kuna wakati mwingine unamuona mtu unahic kama vile unapita daraja la salender....lol
Baeleze mamaaa!
Akina baba/kaka hudhani wao tu ndio wanawachoka wanawake.....hawajui na sisi twawachoka hivyo hivyo...tena labda kuliko wafikiriavyo au kuliko wanavyotuchoka.Fikiria mtu anayekuudhi kila kukicha -mara kapita kona hii na kimada, mara katembea na mfanya kazi wako wa ndani, mara anatembea na sekretari wake, mara analala na muuza baa, mara anaokota changudoa wanamalizana kwenye gari.Akija home anategemea wewe upo tu unamsubiria kama vile yeye ndo samaki pekee aliyebakia baharini.Binafsi sina nafasi na mwanaume kama huyu.Ikitokea sababu tu ya kusepa atanisikia kwenye radio.Atajuuuuuuta! kumfahamu Queen!
 
Wasuluhishi hawahitajiki zaidi ya wawili washitakianao. Nafikiri walengwa ni mke na mume si mtu mwingine.

mahusiano yamenishinda kuelea mpaka leo, ni kitendawili. Ninachoona mimi bora mtu ukae kivyako kuliko kuingia sehemu ambayo utawahi kuchoka au vitimbi vingi ili muachane.

Siku hizi waume kwa wanawake wote tumekuwa vichaa tu hakuna mwenye akili timamu. Mtu akipata ki nyumba kidogo nje anaanzisha tabia ambayo mwenzie hawezi vumilia ili mmoja awe na maamuzi ya kuacha mwenyewe. Hili nalipinga sana kwa sababu unavyoniacha kwa style hiyo make sure mpya hajui akijua anakumwaga kwa style hiyo.

Tujifunze kupendana jamani, tumake difference. Ukiesema bora ukae bila kuolewa au kuoa kwa sababu mnachokana kweli ni makosa anyway sitaki kuhukumu. tufudishane njia za kufanya kuridhishana, maana hata huko unakoenda hujui kama hizo huduma zitadumu au la. Inaniuma sana tunafanya maisha kuwa magumu.
 

...ndoa ni kama kiatu tu, kikikubana au kukupwaya weye ndiye mvaaji. Kiatu kinastiri siri ya mguu, hata kama umeking'arisha na polish ilhali soksi ndani imetoboka, wewe ndiye mwenye mwamuzi..

Kutafutana shari au amani ndani ya ndoa ni chaguo lako wewe (mvaaji). Hakuna mpatanishi wala msuluhishi atayewapatanisha iwapo mwenyewe 'hutaki!'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…