Kutapika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutapika

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 18, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kutapika kwa kawaida ni dalili ya kuonyesha kuwa, kuna shida tumboni, umekula chakula kilichoharibika au una mafua.

  Unapoumwa sana na kichwa na kupata shida zingine za kiafya, au uja uzito, vinaweza kumfanya mtu atapike. Mara nyingi kutapika sio hoja lakini nyakati zingine, ni muhimu mtu aende atazamwe na daktari.Kuna uwezekano kwamba, unapotapika sana unaweza kuishiwa na maji ya kutosha mwilini.
  Namna ya kutibu kutapika:

  • Nusu saa au saa moja baada ya kutapika, kunywa maji kidogo kidogo ama vinywaji visivyo vileo.Usinywe mara moja au kwa wakati mmoja.
  • Pumzika vya kutosha
  • Baada ya tumbo kutulia jaribu kula vyakula vigumuvigumu kama vile mkate mkavu ,ndizi au kitu kizitozito na kitamu kama halua.
  • Meza dawa ya kuzuia joto na maumivu ya mwili ya Panadol au Tylenol.
  Muite daktari iwapo:

  • Unaishiwa na maji mwilini.Ukisikia kiu sana , midomo kukauka, mgonjwa kukojoa mkojo uliokolea na huwa anahisi usingizi au kizunguzungu ama huhisi kichwa kikiwa chepesi mno.
  • Shingo kuwa gumu lisiweze kugeuka
  • Unatapika zaidi ya mara kumi kaw siku ama ushindwe kumeza maji yoyote pasipo kutapika.
  • Unahisi maumivu makali ya kifua
  • Utapike damu ama vitu vinavyofanana na kahawa iliyosagwa.
  • Unatapika ukiwa na joto jingi la nyusi 38oc au zaidi ya hapo kwa zaidi ya siku mbili.
  • Unatapika kwa zaidi ya Juma moja .
  • Unashtukia tu ukiwa na maumivu makali ya tumbo ambayo huendelea kuwa machungu.
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuna rafiki yangu mmoja wa kike huwa anapo-bleed ile siku ya kwanza dakika chache kabla ya bleed kuanza anatapika.

  Je hili ni tatizo? Au wa/m-kubwa mu/u-nalielezeaje hili!
  Thanx
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  inategemea wanawake wengine huwa wanatapika wakiwa wanapata siku zao za mwezi lakini sio wote ikizidi zaidi ya siku moja bora uende kwa Doctor akupatie dawa ya kuzuia kutapika.
   
Loading...