Mkuu sio kama ninakusema vibaya ila mmezidi sana, yaani huwa mnaona mkitoa hizo laki mbili au tano kumpatia wakili huwa mnaona kuwa mtafilisisika na ukute upo hapo Dar miaka na miaka na una elimu ya chuo kikuu.
Humu JF ulipokuja kuomba ushauri huu kuna nyuzi nyingi sana za tahadhali za kuchukua unaponunua viwanja lakini nadhani na wewe ulikua kwenye ule mkumbo wa 'mwenye hela hashauriwi'.
Acheni uzembe na matumizi ya hela zenu pale mnapojua kuwa likiharibika litakuumiza, ona sasa laki tano ambayo ungempa wakili inakuingiza kwenye maumivu ya mamilioni na hapo ukute ndio mmeingia ile mikataba ya kwa mwenyekiti wa mtaa๐๐๐๐๐๐ mbona patamu hapooo.
NINI UFANYE?
Nenda polisi ukapeleke malalamiko ya wizi wa kuaminiwa yaani umetapeliwa unataka kurudishiwa hela zako. Na siku nyingine ukitaka kununua hayo maeneo ya namna hiyo hakikisha unawapata mashahidi wa pande zote zinazopakana na hilo eneo unalotaka kununua itakusaidia kuepusha migogoro ya kimipaka na kiumiliki, pia fanya uchunguzi kujua umiliki halali wa eneo husika