Kutana na Carlos enriquê Raposo aka Kaiser

FananiMedia

Member
Jul 29, 2021
28
83
AUTH: FANANI MEDIA

Jukumu la mchezaji wa pila wa miguu anae cheza eneo la mshambuliaji ni kufunga mabao. Jukumu ambalo litasaidia timu kushinda mechi na mashindano hakuna ushindi kama hakuna mgoli kwenye mpila wa miguu.

Ikiwa mchezaji wa eneo hili atashindwa kutekeleza jukumu hilo vizuri, inamaanisha mchezaji huyo hafai kwa nafasi hiyo na timu haimuhitaji.!

Hii kweli kwa wachezaji wote Duniani ispokua kwa Carlos Enrique Raposo al maaruf kama Kaizer

Huyu ni wachezaji ambae alikiuka dhana hii ya kawaida na ilio zoeleka miaka na miaka karne na karne kua ili uwe mshambuliaji kwenye mpila wa miguu ni lazima ufunge mabao alaf sifi maisha yakaenda kwa mikataba minono na kucheza vilabu vikubwa tofauti tofauti

Achana Olivier Giroud mtoto mdogo...! akiwa na kikosi cha ufaransa Kilicho twaa ubingwa wa Dunia mwaka 2018 na kutoka bila goli wala pasi ya goli licha ya kua ni mshambuliaja na kombe alipata....

Viunga vya Carlington Manchester united kuna Legend alie maliza mwaka mzima na miezi bila goli wala pasi ya mwisho akiwa kama mshambuliaji,. Jesse Lingard wa kijiweni wanamuita Lionel Jesse Lingardinhol lakini pia huyo ni mtoto mdogo achana nae...!

Huyu ni Carlos Henrique Raposo anayejulikana kama Carlos Kaiser ni mchezaji wa zamani ambaye alicheza kama mshambuliaji wa vilabu tofauti tofauti katika miaka ya 70, 80 na mapema 90 na kucheza kwa miaka 26 katika vilabu kumi tofauti bila goli wala pasi ya mwisho

Yani Carlos Enqie Raposo amecheza vilabi 10 tofauti kwa muda wa miaka 26 akiwa kama mshambuliaji bila goli wala pasi ya mwisho...
Eeeh ndio!

Mbrazil huyo ingawa alikuwa sehemu ya vilabu 10 katika maisha yake ya muda mrefu ya mpira wa miguu, hakuwahi kucheza mchezo rasmi wowote na pia alificha uwezo wake mdogo kwa kisingizio cha majeraha ya uwongo.

Licha ya ulaghai wake, Carlos aliweza kusainiwa kwa mpaka Ulaya, Amerika na Amerika Kusini kwa kuonesha video bandia za magoli yake bora huku akiwalipa mashabiki kuimba jina lake ili kushawishi vilabu kuamini kua alikuwa nyota wa kweli!

Pia alidanganya wengi kwa kufanya urafiki na waandishi wa habari ambao waliandika makala bandia kumhusu wakimsifia.

Katika nakala moja ya gazeti, ilisomeka kwamba alikuwa hatari sana huko Puebla (moja ya vilabu vya Mexico Carlos alicheza) kwamba alipewa uraia wa Mexico na kuichezea timu yao ya taifa kutokana na uwezo wake kua mkubwa lakini yeye alikataa kumbe uongo mtupu!.

Baada ya kurudi Brazil, alikua rafiki na wanasoka wa wakubwa kama Carlos Alberto Torres, Ricardo Rocha na Renato Gaucho. Kulingana na ripoti, alifanya hivyo ili kuwa na konekseni bora na kuwavutia wamiliki wa vilabu wakati wowote alipotaka kuhamia klabu mpya.

Alitumia pia simu bandia ambazo hazikuwa maarufu zamani, kutengeneza mazungumzo bandia katika lugha za kigeni au kujifanya kukataa ofa feki ili aonekane kua yeye ni bora.

Alifanya hivyo ili atengeneze picha kwamba yeye ni wanoto sokoni. Siku zote alikuwa akipendelea kusaini mikataba ya muda mfupi ili asikamatwe,alikua akifanya mazoezi tu na timu anajifanya majeruhi ili kukosa siku za mechi.

Mnamo 1986, alihamia Ulaya na kujiunga na klabu ya Kifaransa inayo cheza ligi daraja la 2 Gazelec Ajaccio. Wakati wa usajiri wake klabu huyo ilipanga mazoezi mbele ya mashabiki wao ili waone uwezo wa sajiri mpya ,
kwa hofu ya kukamatwa alipiga mipira yote kwenye umati wa mashabiki na kua bize akambusu beji ya kilabu wala asifamye cha maana..

Kisha alirudi Brazil ambapo alijiunga na Flamengo huko pia alijifanya majeruhi tena.

Japo, mdhamini mkuu wa klabu hiyo bwana Castor de Andrade alifadhaika kumuona Kaiser akiwa nje ya uwanja na kumtaka apangwe japo mechi moja ili aoneshe uwezo wake.

Awali, kwenye benchi, Castor alimwambia kocha amweke kikosini Kaiser kwani timu yake ilikuwa imepoteza kwa 2-0 hivyo kumwambia mchezaji huyo kupasha misuli ili akaokoe jahazi.

Tena! aliogopa kukamatwa, aliona kundi la mashabiki wakishangilia wachezaji.akaamua kuanza kupambana nao ili atolewe nje kabla hata ya kuingia uwanjani akafanya sana vurugu na kupigana na shabiki mmoja.

Baada ya mechi, Kaiser alidanganya kwamba mashabiki walikuwa wakimwita baba yake mwizi. Kaiser alisamehewa na akaongezewa miezi sita kwenye mkataba napo hakucheza hata mechi moja baada ya kujifanya maheruhi kama kawaida yake.

Klabu yake ya mwisho ilikuwa Vasco da Gama, na timu nyingine alizocheza ni Puebla, Botafogo, Flamengo, Gazélec Ajaccio, Bangu, Fluminense, El Paso Sixshooters América (RJ) Guarany Futebol Clube

Huyu ndio Raposo Fundi wa kiBrazili alie dumu kwenye soka kwa miaka 26 na vilabu 10 bila kufunga goli wala pasi ya goli.


Subscribe chanel yetu ya Youtube kwa mfululizo wa makala za video na sauti..
 
Back
Top Bottom